Ads

CRDB YAPUNGUZA RIBA



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgcUMWTBMnWwHvfQIS72EIJq1p0P17kUd2TDrMGow8El_aK_o_yHpR-gVdAkPYAilutv7KV9j0Q2qTc3Cdic4SH6ZDCbPgB1FVoUyukA9STIjp5QkW4ywAXTu2jmhpzOCuUGOAMLbx-1viJ/s640/unnamed.jpg
Mwambawahabari 
Bank ya crdb imepunguza riba ya mikopo  kwa wafanyakazi kutoka 22% hadi 16% na kuongeza mda wa marejesho ya mkopo hadi miaka 7           sanjari na hilo bank hiyo imeongeza kiwango cha mkopo kwa wafanyakazi kutoka shilingi million hamsini hadi shilingi million mia moja
         Hayo yamebainishwa jijini daresalama na mkurugenzi mtendaji wa crdb Dr. Charles kimei ofisini mwake amesisitiza kuwa mkopo utatolewa baada ya saa 12 baada ya mwombaji au mkopaji kuthibitika kutimiza vigezo sahihi
         “Tumezingatia ushauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye amezitaka benki zipunguze riba na pia tunapunguzia mzigo wa makato makubwa wafanyakazi kutokana na kuongezeka mda wa marejesho”
            Aidha Kimei alisema na washauri wafanyakazi kama walivyo sasa wanapata usumbufu wa kupigwa penati nendeni benki kuu  kuna kitengo  cha malalamiko na huko sheria zitawalinda
           “Wafanyakazi wa sekta binasfi karibuni waajiri wenu wawe wadhamini ili kuhakikisha mikopo inarejeshwa kwa wakati”
            Kwa upande wake mkurugenzi wa tawi la holand house Bw. Almasi alisema kuzinduliwa kwa huduma hiyo ni chachu ya kauli mbiu ya crdb benki ambayo ni benki inayomskiliza mteja.
             “Wateja wetu tunawapenda na kuwasikiliza tunawajali na kuwathamini karibuni crdb chochote unachohitaji juu ya maswala ya huduma za kibenki tutawasikiliza”. 

No comments