TCRA WATOA LESENI KWA BLOGER.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba akizungumza na wadau mbalimbali wa mitando leo jijini Dar es Salaam
MWAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekabidhi leseni za kufanya huduma ya kutoa habari kwa njia ya mtandao kwa Blogs, Online TV na Online Redio ambazo zimekamilisha usajili na kulipa ada ya leseni.
Zaidi mitandao 45 ikiwemo Blogs na Online TV zimekabidhiwa leseni ya kufanya huduma hizo huku waombaji walikuwa zaidi ya 200 kati ya hao 65 wamefanikuwa kukubaliwa maombi yao.
Akizungumza waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema kuwa zoezi hilo endelevu lina lengo la kuzuia uanzishwaji holela wa blogs na online tv ambazo unazinaweza kusababisha madhara kwa jamii.
“Jambo la kwaza tunazuia uanzishwaji holela wa vyombo vya habari mtandaoni usiokidhi viwango vinavyotakiwa, ikumbukwe kwamba umiliki wa vyombo vya habari bila tozo unaweza ukaleta utitiri wa vyombo hivi na ikawa changamoto katika usimamizi na kwa jamii,” amesema Mhandisi James Kulaba.
Post a Comment