MANISPAA YA ILALA WAJIPANGA KUNYAKUA UMISSETA
Baadhi ya wachezaji wa mpira wa mkono manispaa ya ilala wakiwa katika mazoezi.
MWAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA. DAR ES SALAAM
Manispaa ya Ilala imejipanga kufanya vizuri katika
mashindano ya michezo shule za sekondari (UMISSETA) yanayotarajia kutimia vumbi Mei 26 mwaka huu katika
viwanja vya taifa jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yanatarajia kuzikutanisha timu tano kutoka
wilaya ya temeke, kinondoni, Ilala pamoja ubungo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mratibu wa Mashindano manispaa ya Ilala Mwalimu Haji, amesema kuwa katika mashindano hayo
watashiriki michezo mbalimbali.
Amesema kuwa michezo
hiyo ni pamoja na mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana, mpira wa wavu, mpira
wa kikapu, mpira wa mikono pamoja na sanaa ya kwaya, maigizo na ngonjera.
Mratibu huyo ameeleza kuwa maandalizi yote yamekamilika, huku mei 26 mwaka huu wakitarajia kuingia kambini kwa ajili ya kuanza mashindano hayo.
Amesema kuwa mwaka wa jana katika mashindano hayo walishika
nafasi ya pili kati ya wilaya tano zilizoshiriki, lakini kwa mwaka huu ametamba kuchukua ubigwa katika mashindano yote watakayoshiriki.
Naye kocha wa mchezo wa mpira wa mkono Mbwire Jeremia, amesema
kuwa timu yake ipo katika hali nzuri ya kimchezo na wanatarajia kuleta
ushindani mkubwa jambo ambalo litasaidia kushika nafasi ya kwanza.
Nahodha wa timu ya mpira wa mkono manispaa ya ilala Martin Emmanuel, amesema kuwa kikosi kipo katika mazingira mazuri katika
mashindano hayo.
“Kocha ametufundisha vizuri, tayari ametupa mbinu zote ili
kuhakikisha tunakuwa wa kwanza katika mchezo huu wa mpira wa mkono” amesema
Emmanuel.
Post a Comment