MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA DKT. NDUGULILE UWANJA WA NDEGE WA J.K NYERERE
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akihoji ufanisi wa utendaji
kazi wa moja ya mashine ya kupima na kutambua dalili za mgonjwa mwenye
EBOLA zilizopo Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere jijini Dar
es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisikiliza kwa makini maelezo
kutoka kwa Afisa Afya Mfawidhi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K
Nyerere Dkt. George Ndaki wakati alipofanya ziara katika Uwanja huo
ili kujiridhisha na utendaji na ufanisi wa mitambo ya kutambua dalili
za mgonjwa mwenye EBOLA.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiendelea na Ziara katika Uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere jijini Dar es salaam akiongozana
na mwenyeji wake Afisa Afya Mfawidhi wa Uwanja huo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na watoto Dkt. Faustine akitoa maelekezo kwa Afisa Afya Mfawidhi
wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere Dkt. George Ndaki pindi
alipofanya ziara leo katika uwanja huo.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile
akiwa katika eneo la kupokelea mizigo wakati akiendelea na ziara yake,
kulia kwake ni Afisa Afya Mfawidhi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
J.K Nyerere Dkt. George Ndaki kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa huduma
za kinga Dkt. Khalid Massa
Na WAMJW-DSM
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee
na Watoto imeridhika na maandalizi ya mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa
ya milipuko ukiwemo ugonjwa wa Ebola katika mipaka yote na viwanja vya
ndege nchini
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile
wakati wa ziara yake katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius
Nyerere
Dkt.Ndugulile amesema amefika hapo ili kuangalia
hali ya maandalizi na ufungaji wa mashine za kisasa za utambuzi wa ugonjwa
wa Ebola endapo itatokea mtu mwenye ugonjwa huo
Aidha, alisema wizara imeimarisha mifumo ya ufuatiliaji
wa magonjwa nchini na kuweka mfumo wa kubaini watu wanaoingia kwa kubaini
hali ya joto linaloongezeka kwa mgeni anayeingia na kufanyiwa uchunguzi
zaidi.
"tumeweka mfumo wa kuwafuatilia wale ambao watakua
wamebainika na joto zaidi mahali watakapofikia na mawasiliano yao ili
kujua hali zao na endapo atapata mabadiliko"
Naibu huyo aliongeza kuwa wamewafanyia mazoezi ya
kutosha kwa watoa huduma wa mipakani na viwanja vya ndege na pia kuwapatia
elimu jinsi ya kukabiliana na ugonjwa huo.
Dkt.Ndugulile ameendekea kusisitiza na kuwatia hofu
wananchi kwamba hadi sasa hakuna mtu alobainika kuwa na ugonjwa wa Ebola
na hali ya mipaka ya Tanzania ni salama
Post a Comment