RC MAKONDA APOKEA VIFAA VYA MILIONI 400 KUFANIKISHA UJENZI NYUMBA ZA WALIMU DAR.
Mkurugenzi
wa Kiwanda cha MMI Steel Subash Patel akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya kiwanda cha MMI Steel .
Rc Makonda akipokea Mabati
MWAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amepokea msaada wa vifaa vya ujenzi
venye thamani ya milioni 400 kutoka kiwanda cha MMI Steel kwa ajili ya
kufaniksha ujenzi wa nyumba za walimu.
Akizungumza
katika hafla ya kupokea vifaa hivyo jijini Dar es Salaam Mhe. Makonda amesema
kuwa kiwanda hicho kimetoa msaada wa mabati 15,000 yenye thamani ya milioni 360
pamoja nondo tani 22.
Mhe.
Makonda amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kukamilisha nyumba za walima ili
waweze kufanya kazi katika mazingira rafiki.
“Watanzania
wanapaswa kuiga mfano huu katika kuchangia sekta ya elimu ili mkoa wetu endelee
kufanya vizuri”amesema Mhe. Makonda.
Mhe.
Makonda amesema tayari wameanza kuchukua vifaa hivyo vya ujenzi kutoka
kiwandani kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa nyumba za walimu.
Ameeleza
kuwa kila mtu anatakiwa kuunga mkono juhudi za kiwanda jambo ambalo
litafanikisha maendeleo katika nyanja mbalimbali.
Katika
hatua nyengine Mhe. Makonda amebainisha kuwa kuna makontena 10 ya vitabu ambavyo
vinatarajia kuja nchini kutoka marekani kwa ajili ya mktaba ya kisasa ambayo
itafanikisha maendeleo ya elimu.
“Kuna
makontena 10 ya vitabu pamoja na vifaa vya maabara ambavyo ni msaada kutoka
marekani vinatarajia kuja nchini ”amesema Mhe. Makonda.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha MMI Steel Subash Patel, amesema kuwa
ametoa msaada wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kuchangia sekta ya elimu katika
mkoa wa Dar es Salaam.
Patel
amesema kuwa katika kiwanda chake kuna wafanyakazi 3,000 ambao wana ajira ya
moja kwa moja, huku asilimia kubwa kati yao wanawatoto wanaosoma.
Ameeleza
kuwa kutokana hilo ameona ni vyema kuwachangia katika kufanikisha ujenzi wa
nyumba za walimu.
“Nitaendelea
kutoa ushirikiano katika kufanikisha masula mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo
kazi ya kujenga nyumba za walimu”amesema Patel.
Hata
hivyo Mkurugenzi huyo amesema kuwa atatoa msaada mwengine wa rangi katika
kufanikisha ujenzi wa nyumba za walimu.
Post a Comment