TUCTA KUSHIRIKI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KIVINGINE
Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Rehema Ludaga akizungumza kuhusiana na Kongamano siku ya wanawake, jijini Dar es Salaam.
Mwamabawahabari
SHIRIKISHO
la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) imeandaa kongamano la siku ya wanawake
litakalofanyika machi 7 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake wa TUCTA, Rehema Ludaga amesema
kongamano la hilo ni kuelekea siku ya
wanawake duniani ambayo inafanyika kila Machi 8.
Amesema kuwa
katika kongamano hilo watajadili nafasi ya mwanamke katika mahala pa kazi kuona
changamoto gani wanakutana wanawake wakiwa sehemu za kazi.
Kauli mbiu
ya maadhimisho hayo ni Tathimini ya Unyanyasaji wa kijinsia mahala pakazi.
Katibu Mkuu
waTUCTA, Dk.Yahya Msigwa amesema kila mwaka wanafanya kongamano ila kuweza
kupata mawazo ya wanawake na kuweza kuboresha sehemu za kazi.
Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo anatarajiwa kuwa
Mkuu wa Wilaya, Sophia Mjema.
Post a Comment