BENKI YA BOA YAMKABIDHI MSHINDI WA DAKA MKWANJA MILIONI 10.
Mshindi wa Kampeni ya Daka Mkwanja, Bw. Reuben Kinamhala wa pili kutoka kushoto akikabidhiwa Sh milioni 10 na Meneja Masoko na Utafiti wa Benki ya BOA, Muganyizi Bisheko leo jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya Benki hiyo.
MWAMBA WA HABARI.
HUSSEIN NDUBIKILE, DAR ES SALAAM.
Benki ya Afrika nchini Tanzania (BOA ) imemkabidhi Sh milioni 10 mshindi wa Kampeni ya Daka Mkwanja, Reuben Kinamhala mkazi wa Mwandege Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Akibabidhi fedha hizo leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Masoko na Utafiti wa benki hiyo, Muganyizi Bisheko amesema kampeni hiyo ilianza mwishoni wa mwezi Novemba mwaka jana na kumalizika Februari 26 mwaka huu huku akisisitiza ililenga kusherehekea miaka 10 ya BOA tangu ianzishwe hapa nchini.
“ Bwana Reuben Mteja wa Tawi la Mtoni wilayani Temeke ambaye pia ni Mzee wa Kanisa la Fellowship Pentecostal la Kurasini amejishindia Sh milioni 10 za Daka MKwanja,” amesema.
Amebainisha kuwa kampeni hiyo ililenga kuwaongezea wateja ufahamu na kutambua umuhimu wa kuhifadhi fedha zao benki na kwamba mteja alitakiwa kuweka kuanzia Sh milioni moja kipindi chote cha kampeni.
Amefafanua kuwa hivi karibuni benki hiyo itazindua kampeni nyingine itakayowawezesha wateja zaidi ya mmoja kjishindia fedha ikitarajiwa kuanza Machi saba hadi mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.
Kwa upande wake mshindi wa kampeni hiyo, Reubeni ameishukuru benki hiyo na kubainisha fedha hizo atatzitumia katika majukumumu ya kifamilia ikiwemo kusomesha watoto shule pamoja na kumsiadia mke wake katika shughuli zake za ujasiriamali.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mauzo cha benki hiyo, Linda Mario amewaomba watanzania kujenga utamaduni wa kufungua akaunti kwa ajili ya kuhifadhi fedha zao na usalama.
Amesema Bwana Reuben aliweka fedha kama kampeni ilivyoagiza huku akibainisha hakutegemea kama angeibuka na mshindi.
Post a Comment