Ads

WAMACHINGA WARASIMISHWA KUFANYA BIASHARA KARIAKOO, DC MJEMA AGAWAVITAMBURISHO.


Dc Mjema akizungumza na Wafanyabiashara hao leo jijini Dar es Salaam,kabla ya kufanya zoezi la kuwapatia vitambulisho.
Mkuu wa Willaya ya Ilala(kulia)akimkabidhi mmoja wa wamachinga hao kitambulisho. 
Na Anna Chiganga 
Mwambawahabari

 Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema amegawa vitambulisho vya Taifa, kwa wafanyabiashara wa Kariakoo(WAMACHINGA) Katika Manispaa hiyo kwa lengo la kusaidia kutambuliwa na Serikali pamoja na kwaunganisha wamachinga hao kuwa kitu kimoja.

DC Mjema amefanya zoezi hilo  leo katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam  ambapo wafanyabiashara 1984 kati ya 6140 wamepatiwa vitambulisho vya taifa .

Amesema vitambulisho hivyo vitawasaidia kuwatambuliwa na Serikali na kuweza kuwasaidia katika mambo mbalimbali hususani kupata vibali vya kusafiria kufuata mzigo nje ya nchi na siyo kusubiri kuletewa na Mtu Fulani.

"Nataka muwe mnasafiri kwenda nje ya nchi kufuata bidhaa na hivyo nafahamu vitambulisho hivi mlivyovipata vitawasaidia kukopa fedha za kuendeleza biashara zenu, na kuweza  kupata vibali vya kusafiria kwenda nje ya nchi ili kufuata bidhaa na siyo kusubiri mtu akuletee mzigo "amesema Dc Mjema.

Aidha Dc Mjema amemtaka Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam(RPC), Razaro Mambosasa kuwakamata wanaouza eneo la vizimba vya kufanyia biashara katika mitaa ya Kariakoo.

Amefafanua kuwa wapo  watu wanaouza  vizimba hivyo kwa wamachinga hao jambo ambalo si sahihi kwani barabara hizo ni mali ya Serikali na kuwataka waliochukua fedha za vizimba hivyo kurudisha kabla hatua kali za kisheria hazijachukuliwa.


"Wanouza haya maeneo naomba RPC uwakamate na uwatie ndani kwani Mitaa hii haiuzwi,ni  Mali ya serikali,kwani barabara hizi zimejengwa na serikali, "Amesema Mjema. 

Ameongeza kuwa anafahamu kuwepo kwa viongozi wa serikali wanaochukua fedha kwa ajili ya maegesho ya magari Katika Soko hilo na kumtaka Katibu Tawala Wilaya Ilala, Edward Mpogolo kuwatafuta na kuchukuliwa hatua.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabishara hao, Stephen Lusinde amesema tukio hilo alilolifanya Dc Mjema ni la kihistoria ambalo halijawahi kutokea ivyo wanamshukuru Mkuu wa wilaya hiyo kwa kuweza kuwaona na kuwasaidia kupata vitambulisho hivyo. 

"Tunamshukuru Sana Dc Mjema kwa kutufanikisha kupata vitambulisho vya taifa kwani tukio hili ni la kihistoria tangu tupate uhuru haijawahi kutokea,na tunaishukuru Serikali ya Rais John Magufuli  kwa kutujali sisi wafanyabiashara(wamachinga)wa Kariakoo"Amesema Lusinde. 

No comments