MAUZO SOKO LA HISA YAMESHUKA
MWAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Afisa Masoko Mwandamizi wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) Marry Kinabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mauzo ya Hisa
(Turnover/ Liquidity)
Mauzo kwa wiki
iliyoishia 23 Februari 2018 yalikuwa shilingi
Bilioni 2.3 ikilinganishwa na mauzo ya shilingi bilioni 6.4 kwa wiki iliyoishia
tarehe 16 Februari 2018.
Vile vile Idadi ya
hisa zilizo uzwa na kununuliwa kwa wiki iliyoishia tarehe 23 Februari 2018 ni
hisa milioni 3.3 ikilinganishwa na mauzo ya hisa ya milioni 11.6 kwa wiki
iliyoishia tarehe 16 Februari 2018.
Kampuni zilizoongoza
katika mauzo ya hisa kwa wiki iliyoishia tarehe 23 Februari 2018 ilikuwa kama ifuatavyo:
TBL……………………………………………30%
VODA …………………………………………25%
TPCC……………………………………………22%
Ukubwa Mtaji (Market
Capitalization)
Ukubwa wa mtaji wa
kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko umepanda kwa
Shilingi Bilioni 456 kutoka Shilingi Trilioni 22.4 wiki iliyopita hadi Shilingi
Trilioni 22.95 wiki iliyoishia tarehe 23 Februari 2018.
Ongezeko hilo limetokana na kupanda kwa bei za hisa za KCB
(8%), EABL (7%), DSE (1%) na SWISS (1%).
Ukubwa wa mtaji wa
kampuni za ndani umepanda kwa Shilingi Bilioni 2 kutoka Trilioni 10.143 hadi kufika
Shilingi Trilioni 10.145 wiki hii. Hii ni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa ya
SWISS (1%) na DSE (1%).
Viashiria (Indices)
Kiashiria cha kampuni zote
zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 47 kutoka pointi 2,336
hadi 2,383 pointi hii ikiwa ni kutokana na kupanda kwa bei za hisa za Kenya
Commercial Bank (KCB), East African Breweries Ltd (EABL), Swissport (SWISS) na Dar
es Salaam Stock Exchange (DSE).
Pia kishiria cha
kampuni za ndani yaani TSI kimepanda kwa pointi 1 kutoka pointi 3,868 hadi pointi
3,869 kutokana na kupanda kwa bei za hisa za
Swissport (SWISS) na Dar es Salaam Stock Exchange (DSE).
Kiashiria cha sekta ya
viwanda (IA) wiki hii imebaki kwenye wastani wa pointi 5286 kama wiki iliyopita
Kiashiria huduma za
kibenki na kifedha (BI) wiki hii imepanda kwa poniti 1 kutoka pointi 2,608 kadi
pointi 2,609 hii imechangiwa na kupanda kwa bei za hisa za DSE kwa asilimia 1%
kutoka shilingi 1580 hadi 1600.
Kiashiria cha Sekta ya
huduma za kibiashara (CS) wiki hii imepanda kwa
pointi 2 kutoka pointi 2,462 hadi pointi 2,464 imechangiwa na kupanda kwa bei
za hisa za SWISS kwa asilimia 1% kutoka shilingi 3500 hadi shillingi 3540.
Hati
Fungani (Bonds)
Mauzo
ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 23 Februari 2018 yalikuwa
Shilingi bilioni 64 kutoka Shilingi Bilioni 8 wiki iliyopita ya 16 Februari 2018.
Mauzo haya yalitokana na hatifungani kumi na sita
(16) za serikali zenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 68 kwa jumla ya
gharama ya Shilingi bilioni 64.
Post a Comment