Ads

MANISPAA YA ILALA YATUMIA ZAIDI YA BILIONI 8 KUTEKELEZA MIRADI YA KIMAENDELEO.

Maafisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakizungumza na waandishi wa habari leo jinini Dar es Salaam, kutoka kulia ni Tabu Shaibu akiwa na George Mwakyembe

MWAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imetumia zaidi ya bilioni 8 katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika bajeti ya mwaka 2017/2018 kwa kipindi cha miezi 6 kuanzia mwezi julai hadi Desemba mwaka wa jana.

Akizumgumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Ilala Tabu Shaibu, amesema kuwa halmashauri imetekeleza miradi mbalimbali inayohusisha ujenzi wa vyomba vya madarasa, hostel, ukarabati wa majengo, miundombinu ya barabara  kwa ajili ya kutatua changamoto katika jamii.

Shaibu amesema kuwa fedha hizo zimetokana na mapato ya ndani, huku sh 5,863, 659, 471 zikiwa tayari zimetumika katika ujenzi wa madarasa 37, matundu ya choo 90 pamoja na ukarabati wa majengo.

" Kwa upande wa elimu kwa shule za msingi tumefanikiwa kujenga shule nne mpya kutokana na ongezeko la wanafunzi ambalo limetokana na mpango wa serikali wa kutoa elimu bila malipo" amesema Shaibu.

Ameeleza kuwa katika elimu wamefanikiwa kujenga kujenga madarasa 28 katika shule za msingi Bonyokwa, Mongo ndege Mbondole, Mji mpya, Kibaga, Bangulo huku  madarasa sita yamefanyiwa ukarabati katika sule ya Kinyerezi pamoja na Mchikichini.

 Shaibu amesema kuwa pia wamefanikiwa kuchukua hatua ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi katika shule ya Sekondari Mbondole iliyopo katika Kata ya Msongola ikiwa na lengo la kukabiliana na changamoto ya usafari kwa wanafunzi wanaokaa mbali na shule.


Huduma za Afya.

Manispaa ya Ilala kupitia miradi ya wafadhili imefanikiwa kukamilisha miradi mikubwa ya ujenzi wa hospitali ya Mama na Mtoto Chanika katika kupunguza vifo vya mama na mtoto kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Jengo la Mama na Mtoto limejengwa katika hospital ya Amana kwa ufadhili wa Amsons Group of Campanies ambapo lina jumla ya vitanda 100 na kufanya idadi ya vitanda kutoka 253 na kufikia 353 katika hospital ya Amana.  

Miradi ya Maji.
Katika Sekta ya maji, halmashauri imeaanza hatua ya mbalimbali za utekelezaji katika miradi ya maji ikiwa ni pamoja na ukamilishaji na ukarabati wa miradi ya maji katika Kata ya Minazi, Tabata, Majohe, Vingunguti, Pugu Sekondari, Mkera pamoja na Pugu Station.

Mpaka sasa tayari halmashauri imeanza kutekeleza miradi ya maji ambapo ni pamoja na ujenzi wa kisima cha maji mtaa wa Mkera Kata ya Msongola, Ujenzi wa tanki lenye ujazo wa kuhifadhi maji kiasi cha lita 250,000 katika eneo la pugu kimani, ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 150,000 la kuhifadhi maji katika Kata ya Kisukuru pamoja na miundombinu ya usambazaji maji katika Kata ya Mzinga.


Miundombinu ya Barabara.

Miradi mingi ya barabara inayotekelezwa katika halmashauri ya Minispaa ya Ilala ni uboreshaji wa miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam kupitia mradi wa DMDP kwa kutumia fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia.

Kupitia mradi wa DMDP tayari barabara sita zimeanza kufanyiwa kazi ikiwemo barabara ya Olympio km 0.68, Kiungani Km 0.68, Mburuku Km 0.38, Omari-Londo Km 0.53, Kongo Km 0.28 pamoja na barabara Ndanda Km 0.3 ambapo barabara gharama yake Sh 8,884,643,432.62.


Ambapo imeeleza kuwa halmashauri ilitumia kiasi bilioni 3 kwa ajili ya kulipa fidia waathirika wa maeneo ambayo yanapitiwa na mradi wa DMDP kwa ajili ya kuweza kutekeleza mradi huo.


Katika hatua nyengine imeelezwa kuwa halmashauri imefanikiwa kutumia milioni 300 kwa ajili ya uwezeshaji wa wanawake, vijana na wenye ulemavu na kuwapopesha fedha ili kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira.

No comments