GSM NA DANUBE KUJENGA KIWANDA KIKKUBWA KIGAMBONI,MWIJAGE ATOA BARAKA.
Na. John Luhende
Mwambawahabari
Waziri wa Viwanda na biashara uwekezaji mhe.
Charles Mwijage amesema
Wizarayake itaendelea kushirikiana na wawekeza katika kuwapatia maeneo
na msaada wa kisheria kwa kuwaelewesha sheria za uwekezaji nchini iliwaweze kufanya shughuri zao kwa uwazi na
ilikuleta maendeleo kwa nchi.
‘’kujengwa
kwa kiwanda hiki kutasaidia kupunguza bei
na upatikanaji wa bidhaa hii kuliko hisasa bidhaa inatoka nje ya nchi,
matatizo yapo na uelewa wa watu
unatofautiana hata vidole
vinatofautiana mtu akaipatwa na
matatizo asikate tamaa hakuna mahala ambapo hakuna vikwazo twende kwenye sheria tueleweshane
kusudi tuendelee kuzalisha ‘’ alisema.
Aidha
amesema kujengwa kwa viwanda kwa wingi kutasaidia kujenga uchumi na kuongeza
mapato na walipakodi na amewataka wawekezaji
hao kufikiria kujenga viwanda zaidi nchini .
Kwa upande wake Meneja masoko wa Kampuni ya GSM , Farida Rubanza amesema wana tarajia kujenga kiwanda kikubwa kitakacho
kuwa kina tengeneza samani za ndani
(Furniture) kwa ajili ya kuuza
nchini na kusafirisha nchi mbalimbali duniani.
‘’Sisi GSM na DANUBE tumeona
Nivema tukaungana ilikujenga kiwanda
hapahahapa na tutakuwa tuna pata malighafi hapahapa na kiwanda kikikamilika
tuta kuwa na uwezo wa kuuza
Contener 500 kwa mwezi na tutauza masoko
ya nje na ndani ‘’ alisema .
Rubanza pia ame mshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
mhe. John P.Magufuli na serikali yake kwa
kwa kuweka mazingira Rafiki kwa wawekezaji wa ndani na wa kigeni na
kuahidi kuwa wao kama waekezaji wataendelea
kutoa ajira kwa watanzania.
Katika muungano huu
amesema, wataanzisha DUNUBE home Academy
na watachukua wahitimu wa vyuo nchi na watawafundisha na kuwapatia ajira ndani na nje ya nchi
walikowekeza na wemgine watawa tafutia ajira sehemu mbalimbali.
Naye Meneja wa wa DANUBE
Sayed Habib , amesema DANUBE imejipanua
katika biashara na huko Dubai na nchi za
kiarabu ni moja ya makampuni makubwa na kwamba ushirikianao wao na GSM kutasaidia
kufanikisha , muda si mrefu wanampango wa kufungua biashara sehemu mbalimbali
katika nchi zingine za kiafrica.
Amesema uwekezaji wao wa
kiwanda cha kutengeneza Samani kutakuwa
na manufaa kwa kuwa malighafi inapatatikana kwa wingi hapa Tanzania.
Post a Comment