WAZIRI MKUU AHIMIZA KILIMO CHA KAHAWA.
Mwambawahabari
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Molam Tanzania Limited, Medappa Mg, wakati alipotembelea Shamba la Kahawa la AVIV lililopo kwenye kijiji cha Lipokela Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu yupo Mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa ufafanuzi wa miche ya Kahawa, na mkulima wa zao hilo, Bi ….wakati akikagua kitalu cha miche ya kahawa katika Shamba la Kahawa la AVIV lililopo kwenye kijiji cha Lipokela Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu yupo Mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi miche ya Kahawa, Mkulima wa zao hilo, Remigius Njovu,inayotolewa bure na Kampuni ya Molam Tanzania Limited, kwa wakulima wa zao la Kahawa, baada ya kukagua kitalu cha miche ya kahawa katika Shamba la Kahawa la AVIV lililopo kwenye kijiji cha Lipokela Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu yupo Mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Molam Tanzania Limited, Medappa Mg, wakati akikagua kitalu cha miche ya Kahawa katika Shamba la Kahawa la AVIV lililopo kwenye kijiji cha Lipokela Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu yupo Mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa mashine ya kukoboa Kahawa na Meneja wa Shamba la Kampuni ya Molam Tanzania Limited, Hamza Kassim, wakati alipotembelea Shamba la Kahawa la AVIV lililopo kwenye kijiji cha Lipokela Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu yupo Mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia Wananchi, wakati alipotembelea Shamba la Kahawa la AVIV lililopo kwenye kijiji cha Lipokela Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, Waziri Mkuu yupo Mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
*Asisitiza kahawa iuzwe kwa mfumo wa ushirika
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi wa wilaya ya Songea mkoani
Ruvuma wajikite kwenye zao la kahawa ili wawe na zao mbadala la
biashara.
Ametoa
wito huo leo (Ijumaa, Januari 5, 2017) wakati akizungumza na wakazi wa
kijiji cha Lipokela na vijiji jirani, wilayani Songea mara baada ya
kukagua shamba la kahawa la Aviv Tanzania lenye ukubwa wa hekta 1,990.
“Limeni
kahawa ili mpate fedha sababu zao hili ni la biashara. Kahawa ni
miongoni mwa mazao matano ya biashara ambayo Serikali ya awamu ya tano
imeamua kuyawekea mkazo ili yaweze kuongeza tija kwa wakulima na kuinua
uchumi wa Taifa”.
“Tumeamua
kuweka mkazo kwenye mazao matano ya pamba, kahawa, chai, korosho na
tumbaku kwa sababu yanaleta tija na kuliingizia Taifa fedha za kigeni,”
alisema na kuongeza:
“Tumefanya
tathmini na tumegundua udhaifu mkubwa mkubwa katika usimamizi wa mazao
haya ndani ya Serikali kuanzia ngazi ya Halmashauri.”
Waziri
Mkuu alisema ni lazima wananchi walime zao hilo na viongozi wahakikishe
wananchi wananufaika za zao hilo. Hata hivyo, alionyeshwa kutoridhishwa
na utendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea baada ya kuelezwa kuwa
kampuni ya Aviv Tanzania imezalisha miche milioni moja lakini
iliyochukuliwa na kusambazwa kwa wananchi ni miche isiyozidi 200,000.
“Kampuni
hii imeamua kutoa miche ya bure kwa wakulima, wamezalisha miche milioni
moja lakini hadi sasa imechukuliwa 200,000 tu. Kuna miche zaidi ya
800,000, imebaki, na tena wawekezaji hawa wanatoa elimu bure ya kulima
na kuitunza mikahawa yako,” alisema.
Amewataka
wakulima hao watenge ekari moja hadi tatu kwa kila kaya ili waweze
kulima zao hilo. “Wana Lipokela tengeni ekari moja hadi tatu za kulima
kahawa, tukifanya hivyo suala la fedha kupitia kahawa litakuwa
limekamilika,” alisema.
Amesema
itabidi zao la kahawa liundiwe mfumo maalum wa ununuzi ambao ni wa
ushirika kwa kuzingatia vyama vya msingi (AMCOS) vilivyokuwepo.
Mapema,
akitoa taarifa juu ya shamba hilo, Meneja wa Aviv Tanzania, Bw. Medu
Medappa alisema lengo la kuanzisha mradi huo lilikuwa ni kuhakikisha
wanapata shamba kubwa la kahawa aina ya Arabica nchini Tanzania lenye
viwango vya kimataifa.
Alisema wamekwishatoa ajira kwa Watanzania wapatao 3,000 zikiwemo za moja kwa moja na za msimu.
Alisema
kampuni hiyo imeweza kuchangia miradi ya maendeleo kwenye vijiji vinne
jirani vya Lipokela, Lusonga, Liganga na Selekano. “Hadi mwaka 2017
tuliweza kukamilisha ujenzi wa zahanatio katika kijiji cha Lipokela,
nyumba ya mwalimu katika vijiji vya Liganga na Lusonga, uchangiaji wa
madawati kwenye vijiji vya Lipokela na Lusonga,” alisema.
Alisema
wameweza kuanzisha scheme ya wakulima wadogo wa nje (outgrowers scheme)
kwa wakulima 2,000 ambao wamegawanyika kwenye vikundi 36 katika vijiji
31 ndani ya mkoa wa Ruvuma.
Waziri
Mkuu anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma kwa kutembelea
wilaya ya Mbinga ambako atakagua miche kwenye taasisi ya TACRI,
atatembelea kiwamda cha kukoboa kahawa cha Mbinga (MCCCO), kuzungumza na
watumishi na madiwani na pia kuhutubia mkutano wa hadhara.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JANUARI 5, 2018.
Post a Comment