WAZAZI MBURAHATI SACCOS YAZINDULIWA RASMI , MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA DSM AITAKA NMB KUPUNGUZA RIBA.
Mwambawahabari
Na. john Luhende
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na wananchi
wa mkoa wa Dar es salaam wametakiwa kujiunga katika vyama vya kuweka na
kukopa SACCOS ilikujikwamua kiuchumi na
kuondokana na hali ya utegemezi .
Hayo yamesema na mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi mkoa wa
Dar es salaam Frank Kalokola Kamugisha wakati wa
uzinduzi wa chama cha kuweka na kukopa
, (Wazazi Mburahati SACCOS) uliofanyika
katika ukumbi wa Simba Oil Mburahati jijini Dar es salaam, na akawataka wanachama
wengine wa chama hicho katika maeneo mbalimbali kuiga mfano wa Mburahati.
‘’Mstarajie
kuwa ukiweka pesa leo na kuitoa kesho
kwa mbautapata kitu ,wekezeni kwa wingi ili muweze kukopa fedha za kufanya maendeleo katika biashara zitakazo wainua kiuchumi na siyo kuzitumia kwa starehe au mambo yasiyo ya
maendeleo” alisema Kamugisha .
Aidha amewashukuru wadhamini wa Mkutano huo Benk ya NMB kwa kupunguza masharti ya kufungua akauti na
kupunguza riba kutoka 3% hadi 2.5% ili
wanachama wa SACCOS hiyo waweze kufaidika na Ushirika huo.
Amesema katika kutekeleza Ilani ya Chama kuwa kila kata kuwa na SACCOS yake
itakayo wawezesha wanachama na
wananchi wasiona mitaji kuweza kuweka na
kukopa fedha zitakazowasaida katika biashara kwa maendeleo binafsi na
taifa kwa ujumla.
Wazazi
Mburahati SACCOS , ilianzishwa mwaka 20/Juni 2017 na kupata usaji wake Novemba 2017 kwa usajili namaba DSR 1647, ikiwa na nawanachama
90 na sasa inawanachama300 , akisoma Risala kwa mgeni Rasmi katibu wa Wazazi
Mburahati Engilibert Nyang’ali
amesema, ushirika huo umelenga kutoa
mafunzo kwaviongozi na wanachama juu ya
namna bora ya kusimamia uendeshaji kwa
kupitia semina ili kuweza kujua haki na wajibu wao na kutoa mafunzo ya ujasilia mali kwa wanachama wote.
Kwa upande
wake afisa ushirika wa Manispaa ya Ubungo
Philipo Emmanuel, amewataka viongozi wa Ushirika huo kuwa waadilifu kwa fedha
za wanachama na kueleza moja ya changamoto katika jamii nielimu kuhushu vyama
vya kuweka na kukopa kwa kuwa wananchi wengi hawana elimu ya kutosha .
Post a Comment