Ads

TRA WAPIGA MNADA WA MAGARI KUDAI KODI

MWAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
mnada
Baadhi ya magari ambayo yanapigwa mnada na TRA kupitia kampuni ya Udalali Yono Auction Mart.
IMG_20180120_112141
 Wateja wa  magari wakifatilia kwa makini mnada wa magari
IMG_20180120_121842
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia Kampuni ya Udalali Yono Auction Mart wameendelea kupiga mnada wa magari katika bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kukusanya kodi ambazo zinaitajika katika kufanikisha shughuli za kimaendeleo.

Mnada huo mkubwa umefanyika leo baada ya magari kukaa muda mrefu kwa kile kinachodaiwa wahusika kushindwa kuyalipia kodi na watu kuchangamkia fursa kwa kujitotekeza kutoka mikoa mbalimbali na kufanikiwa kununua magari hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Yono Auction MartScolastica Kevela, amesema kuwa mnada umekwenda vizuri kutokana na idadi kubwa ya wateja kununua magari kwa bei nzuri.

Ameeleza kuwa ununuzi wa magari umefanyika kwa asilimia kubwa na wanaendelea kuwashukuru wateja ambao wamekuwa wakiunga juhudi za serikali za kukusanya kodi kupitia mnada huo.

“Tunawaomba watanzania waendelee kuja pale wanaposikia Yono Auction Mart wanafanya mnada kwa niaba ya TRA kwani kufanya hivyo tutalijenga taifa la Tanzania” amesema Kevela.
IMG_20180120_121924
Gari aina ya Benzi lililonunuliwa kwa sh miloni 15 

mnada
Baadhi ya magari yanayopigwa mnada na TRA

Katika hatua nyengine amebainisha kuwa januari 25 na 27 mwaka huu, katika bandari ya Dar es Salaam kutakuwa na mnada mwengine kubwa wa magari ya aina mbalimbali.

Kevela ameeleza kuwa siku moja kabla ya mnada huo kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa 10 jioni katika eneo la bandari wateja wanapaswa kufika kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa magari hayo.

“Watu wasikatishwe tamaa kuwa mnada huu wa magari una bei kubwa, kwani tumeshudia leo wateja wetu wakinunua magari kwa bei nafuu….tunawaomba waendelee kuja ili serikali ikusanya kodi yake” amesema Kevela

YONO
Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Yono Auction Mart Scolastica Kevela.

No comments