Ads

TRA YA ANZA ZOEZI LA KUSAJILI WALIPAKODI WAPYA, CHANIKA ILALA



Mfanyakajazi wa TRA,akimhudunia mteja katika Kituo cha kuandikisha walipakodi  eneo la Chanika. (Picha na John Luhende).

Na. John Luhende
Mwambawahabari
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imesema kuwa wanatarajia kusajili walipakodi wapya 1000,000  ambao watalipa kodi Sh. Bilioni 1.5.

Akizungumza katika usajili wa kituo cha kusajili wafanyabiashara wa dogo cha Chanika, Kamishna wa Kodi za Ndani, Elijah Mwandumbya amesema kuwa kampeni ya kusajili wafanyabiashara wa dogo ni endelevu.




Kamishna wa Kodi za Ndani, Elijah Mwandumbya, akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la Chanika.(Picha na John Luhende).

Elijah amesema kuwa wananchi Wajitokeze kusajiliwa kadri kodi zinavyolipwa ndiyo zinafanya maendeleo ya nchi.

Amesema kuwa uhamasishaji wa ulipaji kodi na usajili utaendelea kwa kuweka vituo karibu na wafanyabiashara.



Mkurugenzi wa Idara ya elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari,(picha  na John Luhende).

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka hiyo Richard Kayombo amewataka wananchi wa naishi maeneo hayo kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kujiandikisha  na kusema kuwa zoezi hilo katika Kituo hicho Litadumu kwa muda wa juma moja.

"tukitoka Manispaa ya Ilala tuta elekea Temeke na baadaye Tutaendelea kufungua vituo katika maeneo mbalimbali" alisema Kayombo.

Aidha Kayombo amesema, Mamlaka hiyo imeamua kuja na kampeni hii  baada ya kutambua kuwa kulikuwa na usumbufu kwa Wafanya biashara kupata TIN namba, kutokana na umbali kutoka wakazi wa eneo hilo hadi Vingunguti, na sasa wamesomea huduma hiyo na kwamba watakaoandukisha hawana lazima kulipa kodi siku hiyo hiyo.

Pamoja na hayo amewatahadhalisha wananchi kutolaghaiwa na matapeli kwani kazi hiyo inafanya na TRA yenyewe na hakuna wakala aliye pewa kazi hiyo.

No comments