Ads

MOHAMED SALAH MCHEZAJI BORA AFRIKA.

MWAMBA WA HABARI.
Nyota  wa timu ya Liverpool raia wa Misri, Mohamed Salah aliyekuwa akichuama na Pierre-Emerick Aubameyang, na Sadio Mane katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora kwa mwaka 2017, usiku wa kumkia leo ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2017 wa Shirikisho la soka barani Afrika.


Salah alionekana kuitetea vyema timu yale ya Liverpool mnamo mwaka  jana 2017 baada ya kujipatia goli 23 katika mechi 29 baada ya kujiunga katika ligi kuu ya Uingereza akitokea timu ya AS Roma.

Wapinzani wake nao si haba kwani Pierre-Emerick Aubameyang, wakati huo huo, alifunga mabao 31 ya kipekee kati ya michezo 32 katika mashindano yote ya mwisho.

Tuzo hiyo ya shirikisho la soka barani Afrika ilikuwa na orodha ya wachezaji wapatao 24, miongoni mwa hao watatu mwezi Desemba Salah, Aubameyang na Mane walitangazwa kuingia katika hatua ya mwisho ya tatu bora .

Mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka uliopita alichaguliwa na makocha kwa kushirikiana na manahodha wa timu katika kila timu ya wanaume barani Afrika.

Sadio Mane kutoka katika timu ya Liverpool amekuwa mshindi wa pili kwa wingi wa kura, pamoja na nyota mchezaji wa timu ya Dortmund ,aubameyang kushika nafasi ya tatu kwa wingi wa kura.

No comments