Ads

Kamishnawa Bima(TIRA),DK. Baghayo Sagware afunguka maneno haya katika mkutano wa wadau wa Bima



Kamishnawa Bima(TIRA),DK. Baghayo Sagware akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa elimu ya matumizi ya mfumo wa utoaji wa bima kwa bidhaa zinazotoka nje ya nchi (TIIP), kwa mawakala wa bima, wadau wa bima na makampuni ya bima nchini leo jijini Dar es Salaam.

Bima hizo zitalipwa kielekroniki kupitia mfumo ujulikanao kama 'Mfumo wa ukataji wa bima kwa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje(TIIP)'uliozinduliwa Januari mosi, 2018.


Hayo yamebainishwa Dar es Salaam leo na Rais wa IIT, Bosco Bugali wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kutumia mfumo wa kusimamia ulipaji wa Bima kwa mizigo na bidhaa zinazoingizwa nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ya usimamizi wa shughuli za bima (TIRA) na SINBAD.


"Sheria ipo wazi kwasababu kila anayeingiza mizigo hapa nchini anapaswa kulipia bima hapa nchini... Kama hakulipa na ikadhihirika kafanya hivyo sheria inaeleza kwamba faini yake sh milioni 5,"amesema.


Amesema bima hizo zitalipwa kwenye makampuni yaliyosajiliwa ambao ni madalali wa bima, mawakala wa bima na watu wa forodha kupitia mfumo huo .


Amefafanua kila atakayeagiza mizigo ni lazima asajili kwenye mtandao huo ili iwe rahisi kuonekana kwenye makampuni ya bima,TIRA na Mamlaka ya mapato (TRA).


Amesema mfumo huo utaondoa ulaghai ambao watu huandika thamani ndogo ya mizigo ukilinganisha na thamani halisi kwani mfumo huo utaonesha thamani sahihi ya malipo ya bima mtu anapaswa kulipa na kuongeza pato la nchi.


Kwa upande wake Kamishna wa Bima (TIRA), Baghayo Sagware amesema utolewaji wa bima nchini umetokana na kufanyika kwa mabadiliko ya sheria Julia 7,2017 iliyokataza kampuni kununua bima kwenye kampuni za nje.


"Utahakikisha taifa halipeleki fedha nje ya nchi hasa za bima, zote zitabaki ndani ambapo kampuni zitaongeza ajira na kuwekeza, pía utamlinda mtumiaji Wa bima kwani wapa waliopata majanga kushindwa kuwasiliana na kampuni za bima za nje pindi atakapopata majanga huku kinga yake ikiishia bandalini,"amesema.





No comments