Ads

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI AWAOMBA WAKULIMA WA KOROSHO KUWA WAAMINIFU KWA WANUNUZI.

Mwambawahabari
Colnely Joseph
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga Abdala Ulega amewaomba wakulima wa korosho kuwa waaminifu na kuacha udanganyifu kwa wanunuzi kwani kwa kufanya hivyo ni kujiumiza wenyewe na hakuna watakae mkomoa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Mkenge ulega alisema kauli hiyo kufuatia hatua ya mkuu wa mkoa wa Pwani kuagiza kukamatwa kwa Wenyeviti wa vikundi vilivyofanya udanganyifu.

Alisema ni jambo la aibu kwa wanamkuranga kufanya udanganyifu ambao unasababisha kucheleweshwa kwa fedha kutoka kwa wanunuzi kwa kuhofia udanganyifu.

"Fedha za wakulima ambazo wanunuzi wameninua zimeshaingizwa tayari lakini wanunuzi wanatakiwa kujiridhisha na mambo yakikaa sawa mtapewa" alisema

No comments