TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA
- MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA NOTI BANDIA WILAYANI ILEMELA.
KWAMBA TAREHE 01.08.2017 MAJIRA YA SAA
23:00HRS KATIKA BAR IITWAYO THE DREAMS ILIYOPO MTAA WA KONA YA BWIRU
KATA YA KITANGIRI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI
WAKIWA KWENYE DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUMKAMATA RYOBA MANGULE,
MIAKA 27, MKAZI WA IBUNGILO, AKIWA NA NOTI BANDIA SITA (6) ZA SHILINGI
ELFU KUMI ZENYE THAMANI YA TSHS 60,000/=, KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA
SHERIA.
AWALI ASKARI WALIPATA TAARIFA KUTOKA KWA
RAIA WEMA KWAMBA KATIKA MAENEO TAJWA HAPO JUU YUPO MTU MWENYE NOTI
BANDIA. AIDHA BAADA YA KUPOKEA TAARIFA HIYO ASKARI WALIFANYA
UFUATILIAJI HADI ENEO HILO NA KUFANYA MSAKO MAENEO HAYO KISHA BAADAE
WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA AKIWA NA KIASI HICHO CHA NOTI BANDIA.
POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO
NA MTUHUMIWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUHUMIWA ATAFIKISHWA
MAHAKAMANI, AIDHA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WENGINE WANAOJIHUSISHA NA
UTENGENEZAJI NA USAMBAZAJI WA NOTI BANDIA BADO UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU
KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA
WA MWANZA AKIWAOMBA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA
KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WAHALIFU NA UHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA
KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA. PIA ANAWATAKA VIJANA KUACHA TABIA
YA UTENGENEZAJI NA USAMBAZAJI WA NOTI BANDIA KWANI NI KOSA LA JINAI NA
ENDAPO MTU ATAKAMATWA AKIWA ANAJIHUSISHA NA UHALIFU WA AINA HIYO HATUA
STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
Post a Comment