OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAANDAA WARSHA YA MAFUNZO YA KEMIKALI NA TAKA HATARISHI KWA MAZINGIRA KWA MAAFISA SHERIA, MAAFISA FORODHA NA WAKAGUZI WA MAZINGIRA NA UBORA WA BIDHAA.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira
-Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akimkaribisha Mgeni Rasmi
kufungua warsha ya mafunzo ya kemikali na taka hatarishi kwa mazingira
kwa Maafsa sheria na maafisa Forodha. Warsha hiyo imeandaliwa na Ofisi
ya Makamu wa Rais inafanyika mjini Morogoro.
Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu
Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bwana Clifford Tandari akifungua Warsha ya
mafunzo ya kemikali na taka hatarishi kwa mazingira kwa Maafisa Sheria
pamoja na Maafsa Forodha na Wakaguzi wa mazingira na ubora wa bidhaa .
Warsha hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Sehemu ya Wadau waliohudhuria
warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais juu ya kujenga
uelewa kwa Maafisa Sheria, Maafisa forodha na Wakaguzi wa mazingira na
ubora wa bidhaa kutoka Taasisi za Serikali
Mmojawapo wa watoa Mada katika warsha hiyo Bwana Faraja Ngerageza kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akiwasilisha mada.
Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu
Tawala wa Mkoa wa Morogoro akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa
Warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais inayofanyika mjini
Morogoro.
Mgeni Rasmi katika warsha hiyo
Bwana Clifford Tandari pamoja na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu
wa Rais Bwana Richard Muyungi (kulia) wakimsikiliza Mwakilishi wa WWF
Africa Bwana Patrick Chibada wakati wa Warsha hiyo.
…………………………..
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro
Bwana Clifford Tandari amesisitiza kuwa ni muhimu kujenga uelewa kwa
Maafisa Sheria, Maafisa forodha na wakaguzi wa mazingira na ubora wa
viwango Nchini ili waweze kutambua kemikali na taka hatarishi kwa
mazingira na matumizi ya Binadamu. Ameyasema hayo mjini Morogoro wakati
wa ufunguzi wa Warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa
Rais.
Aliongeza kuwa moja ya changamoto
ambayo dunia inaikabili kwa sasa ni usimamizi wa kemikali na taka
hatarishi katika jamii zetu. ” Hizi kemikali na taka zinahitajika
kusimamiwa vizuri ili kupunguza madhara ya afya kwa binadamu na
mazingira na pia Wanawake na watoto wapo kwenye hatari kubwa ya
kuathirika na kemikali hizo na kupeleka magonjwa makubwa hatarishi
yatokanayo na kemikali hizo” alisema.
Bwana Tandari aliwataka Maofisa
walioalikwa kujengewa uelewa wa kemikali na taka hatarishi wakaitumie
elimu hiyo katika majukumu ya kazi zao za kila siku na hivyo kupelekea
usimamizi stahiki wa wa taka na kemikali hizo. Na hiyo itapelekea
kupunguza na kumaliza kabisa athari za kemikali na taka hatarishi katika
Nchi yetu.
Warsha hiyo imeandaliwa na Ofisi
ya Makamu wa Rais – Idara ya Mazingira ili kuwajengea uelewa Maafisa hao
ili kuweza kudhibiti uingizwaji na usambazaji wa kemikali hizo
hatarishi Nchini. Katika Warsha hiyo Maafisa wa forodha, sheria na
wakaguzi wa Mazingira na viwango vya ubora wamehudhuria hivyo basi
uelewa juu ya kemikali hizo utaongezeka na utawasaidia katika majukumu
yao ya kila siku wanapokua makazini.
Post a Comment