KANISA KATOLIKI LAMALIZA KERO YA MAJI MAHABUSU YA WATOTO
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki
Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo (katikati) akisisitiza
jambo kwa wageni waalikwa wakati akikabidhi kisima kwa Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (Kushoto) kwa
ajili ya mahabusu ya watoto mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia
ni Padre Timotheo Maganga Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa Dar es
Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto) akisisitiza
jambo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati akipokea kisima toka
kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali
Polycarp Pengo (katikati) kulia ni Padre Timotheo Maganga
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki
Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo (kulia) akikata utepe
kuzindua kisma cha maji mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kushoto) akifungua bomba
kuashiria kupokea kisima toka kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar
es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo kulia
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto) akisisitiza jambo
kwa wageni waalikwa wakati akipokea kisima toka kwa Askofu Mkuu wa
Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo Mkuu
(katikati) kulia ni Padre Timotheo Maganga
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo
……………………….
Na Agness Moshi na Anthony Ishengoma- Maelezo
Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la
Dar es Salaam leo limekabidhi Kisima chenye thamani ya Shilingi Milioni
kumi na moja laki saba na themanini (Sh. 11,780,000/=) kwa Serikali ili
kutatua tatizo la maji katika Mahabusu ya Watoto iliyoko Upanga jijini
Dar es Salaam.
Akiongea katika hafla ya
makabidhiano ya Kisima hicho Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam
Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo amesema lengo kuu la Mchango wa Kanisa
katika ujenzi wa Kisima hicho ni kuonesha kuwa Kanisa haliko mbali na
Serikali katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.
Alisema Kanisa Katolitiki
Tanzania linashirikiana na serikali katika juhudi zake za kuwaletea
wananchi maendeleo bila kujali itikadi za kidini chama au kikabila ili
kusudi wanapotoka kwenye vituo hivyo watambue wamesaidiwa kutokana na
mapenzi mema ya kanisa hilo kwa watu wote.
Naye Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema ujenzi wa
kisima hicho umesaidia serikali kupunguza gharama ya kulipia bili ya
maji ambayo kwa mwezi mmoja serikali ilikuwa inalipa Shilingi laki nne
kwa ajili ya matumizi ya maji katika mahabusu hiyo.
Waziri Ummy amesema kutokana
na ujenzi wa kisima hicho tatizo la maji limekwisha kwa asilimia mia
moja kwasababu kisima hicho kina uwezo wa kuzalisha lita 5,000 kwa saa.
Aidha amesema kuwa fedha
ambazo zimeokolewa na ujenzi wa kisima hicho zitatumika kwa ajili ya
kuwakatia Bima ya Afya Watoto wanaozuiliwa katika vituo hivyo ili
kuwahakikishia upatikanaji wa matibabu.
Amesema ni muhimu kwa jamii
kufahamu kuwa ni Mahakama tu ndio yenye uwezo wa kutoa amri ya watoto
kuhifadhiwa katika mahabusu hiyo na sio mtu au chombo chochote
kingine.
Waziri Ummy alimwambia
Kardinali Pengo kuwa hapa nchini kuna Mahabusu 5 ambazo ni Mahabusu ya
Watoto Dar es Salaam (Upanga), Mahabusu ya Watoto Tanga, Mahabusu ya
Watoto Moshi, Mahabusu ya Watoto Arusha na Mahabusu ya watoto Mbeya.
Amezitaja huduma zinazotolewa
na Wizara yake kwa watoto walioko kwenye Mahabusu hizo kuwa ziko za
aina tatu ambazo ni uhifadhi na utunzaji wa watoto, huduma za
maadilisho kwa watoto ambao tayari Mahakama imewahukumu, na huduma za
Kijamii za Marekebisho ya tabia kwa watoto waliokinzana na Sheria.
Wakati huo Mkurugenzi wa
Mashirika ya Kipapa Kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mwakilishi
wa watoto na vijana wainjilishaji mtandaoni Padre Thimotheo Nyasulu
amesema kuwa, wameamua kutoa msaada huo baada ya kuona changamoto hiyo
walipotembelea kituo hicho Desemba ,2016 kama sehemu ya matendo ya
huruma kwa kanisa.
Aidha Padre Nyasulu ametoa rai
kwa Wananchi na waandishi wa habari kutoendelea kuita vituo vya watoto
waliokinzana na Sheria Mahabusu na kushauri viitwe vituo vya malezi
kwasababu hali hiyo inawafanya kujiona wametengwa hali inayowaongezea
adhabu.
Waziri Ummy alisema Mahabusu za
watoto ni moja kati ya huduma kongwe hapa nchini mahususi kwa
kuwahifadhi watoto walio kinzana na Sheria na ambao kwa sababu moja au
nyingine hawakuweza kupata dhamana kwa kesi au mashauri ambayo
yanawakabili Mahakamani.
Post a Comment