KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUUNDA KAMATI ZA ULINZI WA WATOTO KUANZIA NGAZI YA MTAA.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya
Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga(kushoto) akisalimiana na mjumbe wa
Kamati Kuu ya Baraza la Watoto Taifa Lulu Nziku mara baada ya kumaliza
mkutano na Baraza la kata ya mseke iringa Vijijini hivi karibuni.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW.
Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WAMJW
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya jamii, Jinsia wazee na watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya
jamii) Bibi Sihaba amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii katika halmashauri
zote nchini kutekeleza wajibu wa uundaji wa Kamati za Ulinzi na Usalama
wa mtoto kuanzia ngazi ya mtaa mahali walipo wananchi ili kuwa na mfumo
thabiti wa kuzuia na kutoa huduma kwa watoto wanaofanyiwa ukatili.
Ameyasema hayo mapema wiki hii
wakati wa kikao cha majumuhisho kwenye kilele cha safari yake ya kikazi
katika kijiji cha Tanangozi, kata ya Mseke, tarafa ya Mlolo, wilaaya ya
Iringa vijijini mkoani Iringa na kupokea taarifa za utetezi wa haki za
watoto kutoka kwa Baraza la Watoto la Kata ya Mseke, Kamati ya Ulinzi na
Usalama wa Mtoto, na Timu ya malezi ya watoto wa Kata ya Mseke.
Ameongeza kuwa mabaraza ya watoto
yakianzishwa na kuimarishwa katika ngazi za vijiji na kata yatasaidia
kutoa raghiba ya watoto kujitambua, kujithamini na kujilinda dhidi ya
vitendo vya ukatili na pia kujiepusha na vishawishi vya mahusiano na
wanaume katika umri mdogo.
Aidha, Katibu Mkuu aliwapongeza
wajumbe wa vyombo hivyo vilivyoundwa na watoto na wazazi kuendeleza
wajibu wao wa kuzuia na kutokomeza ukatili na nyanyasaji wa watoto
katika ngazi ya familia, jamii na shuleni ili kuongeza ubora wa jamii
zetu katika utoaji wa haki za msingi za watoto wote katika jamii zetu.
Alisema Serikali imekamilisha
mwongozo wa utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza dhidi ya
wanawake na watoto hapanchioni amabo utasambazwa kwa wadau ili kutoa
maelekezo fasaha ya utendaji katika maeneo ya utekelezaji wa Serikali
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga
amesisitiza kutumia vikundi vya malezi ya watoto na sanaa katika Kata
ya Msewe, Wilaya ya Iringa Vijijini kwa kujiunga pamoja na kutumia stadi
na mbinu walizonazo katika kuelimu jamii kuacha vitendo vya ukatili
dhidi ya watoto ili kuimarisha mazingira upatikanaji wa haki na usawa
kwa wototo wote.
Post a Comment