MBUNIFU WA JIKO LA GES LA GHARAMA NAFUU ALIYE PANIA KUNUSURU MISITU NA MAZINGIRA AWATAKA WATANZANIA KUACHANA NA KUNI NA MKAA.
Na John Luhende
mwambawahabari
mwambawahabari
Dunia sasa
inapita katika mabadiliko ya hali ya tabia ya nchi ambapo hali hiyo kwa mujibu
wa wataalaamu wa mazingira wanasema hali hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na
shughuli za kibinadamu.
Shughuli
hizo ni pamoja ukataji miti holela kwaajili ya mbao , kuni ,mkaa na shughuli za
kilimo ambazo hufanywa katika vyanzo vya maji, ukiacha uchafuzi mwingine ambao
hufanywa na viwanda vikubwa ambavyo navyo huzalisha hewa ya ukaa na kemikali
ambazo huchafua hewa na vyanzo vya maji na kuathili viumbe hai na mimea.
Inocent
Kazungu ni mwanamazingira na mbunifu wa
jiko sanifuni ambalo hutumia ges, anasema suala la kutunza mazigira ni muhimu
sana
“Nimebuni jiko jiko hili nimelipa jina la Cooker take away na jiko lapilli
nimelipa jinala Kazungu ges (mwendo kasi) majiko hayo yana rahisisha sana kazi
za kupika na nigharama nafuu sana mtungi wake mgogo ni kuanzia shilingi
2000tu. naomba watanzania tuachane na kuni na mkaa tutunze mazingira yetu” Alisema mbunifu huyo.
Amesema
lengo la kubuni hili jiko ni kuokoa misitu ambayo kila siku ime endelea
kuteketea kwaajili ya kuni na mkaa wa kupikia
na sasa jiko hili lita kuwa mbadala
wa nishati nhiyo na lina tumia gesi asili ya hapahapa nchi na anashukuru
serikali kwa kutambua mchango wa wabuni
wa majiko na wanachi wameelewa kuwa nia yetu ni njema kuokoa misitu yetu .
“Naishukuru
serikalikupitia NEMC imenipeleka sehemu
nyingi sana ikiwemo katika maonyesho ya sabaaba Dar es salaam , Nanenane Lindi
na katika siku ya mazingira Dunian ambayo yalifanyika Butiama katika mkoani Mara na kote huko
nimetoa elimu ya kutunza mazingira na matumizi ya jiko langu na nina shukuru
sana watanzania wamelipokea kwa vizuri na mahitaji yamekuwa makubwa” alisema Kazungu
Pamoja na
hayo anasema changamoto kubwa kwa wabunifu wa kitanzania imekuwa ni mtaji wa
kuendeleza ubunifu wao anasema anapata
wateja wa majiko kutoka mikoa mbali mbali laiki anashindwa kukidhi mahitaji ya
soko kwa kuwa hana mtaji wa kutosha lakini anaimani kuwa kwa kipindi hiki
ambapo serikali inahimiza kuanzisha kwa viwanda watapata uungwaji mkono kutoka
serikalini ili kuwaeza kuwa na viwanda vidovidogo.
Kwa mahitaji
yako ya jikobora la ges lenye
gharama nafuu Kazungu anapatikana
Vingunguti sido au wasiliana naye kwa companykazungu@gmail.com na
0673899222.
Post a Comment