JPM KUWASILI TABORA JUMAPILI-RC TABORA
Mwambawahabari
Na Tiganya Vincent-RS_TABORA
Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kesho 
tarehe 23 Julai 2017 ,anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili mkoani 
hapa  kwa ajili ya uzinduzi wa miradi ya mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza
 na waandishi wa habari jana Ofisi kwake Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. 
Aggrey Mwanri alisema Mhe. Rais Dkt.Magufuli atawasili mkoani Tabora 
akitokea Kigoma ambapo wanatarajia kumpokea katika Wilaya ya Kaliua siku
 ya Jumapili .
Alisema
 kuwa mara baada ya kuwasili Wilayani Kaliua kuzindua uzinduzi wa 
barabara kutoka Kaliua hadi Kazilambwa na baadaye atapata fursa ya 
kuwahutubia wananchi.
Bw.
 Mwanri aliongeza kuwa akiwa njiani kuelekea Tabora Mhe Rais Magufuli 
atazinduza barabara ya Urambo hadi Tabora siku hiyo hiyo na ambapo pia 
atawahutubia wakazi wa Urambo na kisha kuelekea Tabora.
Alisema
 kuwa siku ya Jumatatu Rais ataweka Jiwe la Msingi ujenzi wa mradi wa 
maji kutoka Ziwa Victoria kuja katika miji ya Nzega , Igunga na Tabora 
na baadae kuzindua upanuzi na ukarabati wa njia za kurikia Ndege katika 
Uwanja wa Tabora.
Mkuu
 huyo wa Mkoa wa Tabora aliongeza kuwa siku hiyo hiyo ,Rais wa Jamhuri 
ya Muungano wa Tanzania  atazindua barabara ya Tabora hadi Nzega na ile 
ya Tabora hadi Nyahua  na mchana atawahutubia wakazi wa Tabora katika 
Viwanja vya Chipukizi.
Alisema
 ujio wa Rais Magufuli kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora ni sawa na usemi 
usemao Mgeni Njoo Mwenyeji Apone kwani zara yake mkoani hapa inazidisha 
matumaini kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora na jirani zake ya kuendelea 
kufunguka milango au fursa mbalimbali za uchumi baada ya kuzindua miradi
 mbalimbali ya miundo mbinu.
Bw. Mwanri alitoa wito kwa niaba ya wananchi wa Tabora kuwakaribisha wananchi kujotokeza kwa wingi  kumlaki na kumsikiliza Rais Magufuli.
Post a Comment