MZAZI ATAKAYEMRUHUSU MTOTO WAKE KUSHIRIKI KAMARI KUSHTAKIWA
Na:
Lilian Lundo – Dodoma
Mtu
yeyote atakaye ruhusu mtoto chini ya miaka 18 kushiriki, kuingia au kukaa
karibu na eneo la mchezo wa kubahatisha (kamari) anahesabiwa kufanya kosa.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini
Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge Viti Maalum Asha Abdullah Juma juu ya
kuongezeka kwa maduka ya kucheza Kamari yanayojulikana kama Jack Pot katika
miji mingi hapa nchini hivyo kusababisha uvunjifu wa maadili na nguvu kazi ya
vijana.
“Michezo
yote ya kubahatisha ikiwemo kamari (slots machines) inaendeshwa kwa mujibu wa
sheria ya Bodi ya Michezo ya kubahatisha namba 4 ya mwaka 2003, sura 41 pamoja
na Kanuni zake,” alifafanua Dkt. Kijaji.
Aliendelea
kwa kusema kuwa, kwa mujibu wa sheria hiyo hakuna mtu au taasisi inayoruhusiwa
kuendesha biashara ya michezo ya kubahatisha bila kuwa na leseni kutoka Bodi ya
Michezo ya kubahatisha pamoja na vibali vingine vinavyotolewa na mamlaka
nyingine za biashara.
Vile
vile sheria hiyo inakataza watoto wenye umri chini ya miaka 18 kushiriki,
kuingia, kukaa au kuzururazurura karibu na maeneo ya michezo ya kubahatisha.
Aidha
mtu yoyote ambaye atamruhusu mtoto chini ya miaka 18, kushiriki, kuingia au
kukaa karibu na eneo la mchezo wa kubahatisha anahesabika kufanya kosa na
anastahili kulipa faini ya shilingi 500,000 au kifungo kisichopungua miezi
mitatu au vyote kwa pamoja.
Dkt.
Kijaji amesema kuwa ikiwa kosa hilo litafanywa na mwendesha mchezo wa
kubahatisha, Bodi inamamlaka ya kumfutia leseni.
Hivyo
basi, wajibu wa Serikali ni kuzuia watoto na vijana walio chini ya miaka 18
kucheza michezo ya kubahatisha.
Pia,
Dkt. Kijaji ametoa rai kwa wazazi na walezi kuwazuia vijana wao kucheza michezo
ya kubahatisha pale wanapoona kuwa uchezaji wao unakuwa na matokeo hasi.
Hata
hivyo amesema kuwa, michezo hiyo inaendeshwa kwa mujibu na sheria kama shughuli
nyingine. Jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa, wanaoendesha michezo hiyo
wanazingatia sheria na kanuni zilizowekwa pamoja na wazazi, walezi na jamii
kuhakikisha vijana wanazingatiia mila na desturi zinazolinda maadili ya
Kitanzania wanapokuwa wanajishughulisha na shughuli halali za kiuchumi.
Post a Comment