Ads

DIVINE WORSHIP KUTOA MSAADA KATIKA KITUO CHA KITAA HOPE CHILDREN HOME

Image may contain: 1 person, outdoor

Mwanzilishi wa Divine Worship Joshua Ngoy Ngoy ama wengine wanavyomfahamu kama Joshua music kama anavyoonekana hapo pichani .

 Na.Veo Ignatus Arusha/Kilimanjaro

Divine Worship imejiandaa kutembelea kituo cha watoto yatima na wajane kilichopo Manispaa ya Moshi mjini Mkoani Kilimanjaro kiulikanacho kama Kitaa Hope Children Home wakiwa na lengo la kuwatembelea na kuzifahamu changamoto mbalimbali wanazopitia watoto hao pamoja na wakina mama hao wajane .

Hayo yamesemwa na mwanzilishi wa kundi la Divine Worship Joshua NgoyNgoy  ambapo amesema kuwa wameamua kutenga siku maalumu kukitembelea kituo hicho ili kuwaonyesha upendo kwa watoto hao, ili na wao  wajisikie ni binadamu wengine"tutakaa nao,tutakula nao pamoja ikiwezekana hata kucheza nao kwa pamoja ili na wao wajisikie faraja na kuwa jamii inawakumbuka pia"

Aidha amesema kuwa hawa watoto yatima na wao wanahitaji kujisikia vizuri kama watu wengine wanavyojisikia.

"Yatima hawa na wajane wanatamani na wao wawe na maisha mazuri kama yale unayoishi wewe hivyo basi tuungane kwa pamoja kwenda kuwatembelea watoto hawa ,ukiwa na chakula ,mavazi,,pesa kiasi chochote tuungane kwa pamoja tukawatembelee naomba sapoti yenu kukitembelea kituo hichi,kwani jambo kama hili tukifanya kwa moyo linampa Mungu utukufu" alisema Joshua.


 Amesema siku ambayo wameitenga ni tarehe 18 februari ambapo itakuwa siku ya jumamosi saa nne asubuhi, hivyo amewaomba watanzania wote ,makampuni mbalimbali pamoja na wadau mabalimbali ili kuwasaidia watoto hawa pamoja na wajane waliopo  kituoni hapo.
Image may contain: 2
people, people sitting and indoor
Muanzilishi wa Huduma ya Divine Worship akiwa katika moja ya ibada kama inavyoonekana pichani
Sambamba na hayo Joshua amesema kuwa ifikapo juni mwaka huu wanatarajia kufanya tamasha la shukurani (thanks giving)tangia kuamnzishwa kwa huduma hiyo ya Divine Worship inayohusika na kuandaa ibada halisi ya kumsifu Mungu.

Aidha amesema kuwa huduma hiyo ilianzishwa 26june2016 ikiwa na lengo la kuwaunganisha waimbaji pamoja na wapigaji vyombo mbalimbali wakiwa na lengo moja la kumsifu Mungu kwa kila mmoja kwa nafasi yake bila kujali madhehebu wala kabila la la mtu ili hali tu ni kiungo katika mwili wa Kristo.

Muanzilishi wa Divine Worship akiwa anafuatilia jambo kwa makini katika mojawapo ya Ibada

Baadhi ya waimbaji wa huduma ya Divine Worship wakiwa jukwaani wanaimba.
 

Waimbaji wa huduma ya Divine Worship Kama wanavyoonekana pichani wakihudumu .

Amesema kuwa mwaka huu wamejipanga kivingine wanayo malengo nya kufikia Tanzania yote na nje ya nchi kwaajili ya kumsifu Mungu, kuwafikia watu wa rika zote.

"Hatusemi hakuna watu wanaomuabudu Mungu katika roho nakweli wapo na wapo waliotutangulia na tunawaheshimu, ila kila mmoja anafanya kwa namna ambayo Mungu amemuagiza kufanya bila kumbagua mu yeyote yule ilihali akijua anafanya kwaajili ya kumsifu na kumtukuza Mungu na wala siyo kwa matakwa yake wala mwanadamu yeyote yule"alisema.

Hadi sasa tangia kuanzishwa kwa huduma ya Divine Worship mwaka jana 2016 tayari wameshafanya ibada mbili ambapo itakapofika june mwaka huu watakuwa wametimiza mwaka mmoja katika huduma hiyo.

No comments