Ads

RC MAKONDA AWATAKA WAKAZI WA DAR ES SALAAM KUJITOKEZA KATIKA UZINDUZI WA MABASI YA MWENDOKASI UTAKAO UZINDULIWA NA RAIS DR MAGUFULI JAN/ 25.

Image result for picha za paul makonda

Na John Luhende 
mwambawahabari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mh Paul Makonda  amewataka  wana nchi wa Mkoa wa Dar es salaam, kujitokeza  kwa wingi kesho katika ufunguzi rasmi wa sehemu ya kwanza ya mradi wa mabasi ya  mwendo wa haraka /mwendo kasi  DART , utakao fanywa kesho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe.Dr John P Magufuli kesho January 25.

Amesema  uzinduzi huo utakuwa ni mwendelezo wa jitihada kubwa zinazo fanywa na serikali katika kutatua kero mbalimbali za wananchi hasa  katika kupunguza msongamano barabarani hapa mjini.


Mradi wa usafiri wa mabasi ya mwendo kazi ulianza kutumika kwa kibali maalumu cha Rais  Magufuli tangu tarehe10/5/2016 kwa safari za kumara ,kivukoni ,morocco ambazo zinahusisha  jumla ya kilomita 20.9 Ikiwa ni sehemu ya kwanza ya mradi huu

Ufunguzi huo utafanyika kuanzia saa 8:00 asubuhi katika kituo cha DART Gerezani kariakoo.

No comments