Ads

CHAKUA YAIOMBA SERIKALI KUKAZIA MATUMIZI YA MFUMO WA ELECTRONICS SEKTA YA USAFIRISHAJI


Image result for PICHA ZA MABASI UBUNGO


Na maria Kaira 
Mwambawahabari
Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA) kimeiomba serikali pamoja na mamlaka zinazosimamia sekta za usafirishaji kuzishinikiza, kuwabana na kuwaelimisha wadau wote wa sekta ya usafirishaji hapa nchini kutumia mfumo wa electronic katika mabasi yaendayo mikoani.

Ombi hilo limetolewa leo hii jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti Taifa wa CHAKUA Hassan Mchanjama  wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema chama chao kimefatilia kwa ukaribu mfumo huo na kubaini kuwa utakuwa na manufaa makubwa kwa abiria waendao mikoani ambapo kila abiria  atatozwa nauli elekezi iliyodhibitishwa na Sumatra.

Mchanjama amesema mfumo huo utaweza kuwanufaisha abiria kwa kuokoa muda wao wa kwenda kwenye vituo vya mabasi na kukata tiketi na badala yake ataweza kukata tiketi ata akiwa nyumbani.


"Mfumo huu utaweza kupunguza utapeli wa kuongeza nauli kipindi cha sikukuu na kipindi cha wanafunzi wanaporudi mashuleni, Pia mfumo huu utawarahisishia abiria kukata tiketi akiwa nyumbani kwa kutumia simu ya mkononi" amesema

Pia amesema kupitia mfumo huo utaweza kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu za abiria pindi inapotokea ajali ili kuweza kujua abiria wangapi waliopata ulemavu, kupoteza maisha pamoja na waliopoteza mali zao.

Aidha Mchanjama amesema  mfumo huo utachangia kupunguza malalamiko kutoka kwa abiria,pia serikali itaweza kujipatia kodi moja kwa moja kupitia Mapato yaliyopatikana katika vya usafiri kulingana na idadi ya abiria waliokuwepo katika basi husika.

Hata hivyo ameongeza kuwa chakuwa haiwezi kufanya kazi peke yake bila uwepo wa jeshi la polisi, pia wamekuwa wakitoa elimu kwa abiria kujua haki zao na wajibu wao .

No comments