Ads

ZIARA YA MFALME WA MOROCCO NCHINI KUKUZA DIPLOMASIA YA UCHUMI



Image result for picha za balozi mahiga

Na. Immaculate Makilika, 
mwambawahabari

Serikali imesema kuwa ziara ya Mfalme wa Morocco nchini Mohammed  wa VI ina lengo  la kukuza diplomasia ya uchumi kati ya nchi hizi mbili, na kamwe haitaathiri  msimamo wa Tanzania katika mgogoro unaoendelea kati ya Morroco na Sahara Magharibi.

Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambapo taarifa hiyo imesisitiza kuwa ziara hiyo itakuza ushirikiano katika masuala ya uchumi.

“ Lengo la ziara hiyo ni kukuza zaidi uhusiano kati ya Tanzania na Morocco hususani katika masuala ya kiuchumi na kibiashara kwa faida ya watu wa nchi hizi mbili, na kamwe  haitaathiri msimamo wa Tanzania katika mgogoro unaoendelea kati ya Morocco na Sahara Magharibi”.


Hata hivyo taarifa hiyo imesisitiza kuwa , msimamo wa Tanzania ambao umekuwa ukisimamiwa na Awamu zote za uongozi  zilizopita na Awamu hii, upo sambamba na ule wa Umoja wa Afrika (AU) unaoutaka Umoja wa Mataifa (UN) ambao ndio wamepewa jukumu la kusimamia mgogoro huo, kuongeza kasi ya kutatua mgogoro huo ili  kupata suluhu ya kudumu.

Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco anatarajiwa kuwasili nchini Oktoba 19 mwaka huu kwa ziara ya siku nne, ambapo atatembelea Zanzibar pamoja na Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajli ya kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Aidha, mara baada ya kumaliza ziara yake nchini, Mfalme Mohammed VI atatembelea nchi za Rwanda, Ethiopia na Kenya.

No comments