Waziri Mkuu apokea misaada ya waathirika wa tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera
mwambawahabari
2084:Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea msaada wa mablanketi kutoka kwa Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida ukiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.Kulia ni Mwakilishi Mkuu wa Shirika la JICA nchini Toshio Nagase.
2101: Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 6.7m kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi Taasisi ya wakaguzi wa ndani wa Serikali na kampuni Binafsi Bw.Richard Magongo leo Jijini Dar es Salaam ukiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
2109: Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea pesa taslimu shilingi milioni 2 kutoka kwa Mwenyekiti wa Magereji Tegeta Bw.Lenard Mwanjela ukiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
2124: Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 325 kutoka kwa wawakilishi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya ACACIA ikiwa ni kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
2140: Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 41.5 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) Bw.Ayoub Ryoba ikiwa ni kutokana na harambee iliyofanywa na Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
2196: Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea moja ya misaada kutoka kwa Katibu wa Jumuiya ya wafanyabiashara wa kariakoo Bw.Abdallah Mwinyi ambao wametoa vifaa vyenye thamani ya milioni 60 ikiwa ni kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
Picha na Daudi Manongi,MAELEZO.
Post a Comment