Ads

DR CHUWA :AGAKHANI NI HOSPITALI BORA, ACHENI MAZOEA YA KWENDA INDIA





Na:John Luhende 
mwambawahabari
Hospitali ya Agakhani  ya jijini Dar es salaam,  imewataka wananchi  kuziamini Hospitali za hapanchini kwa kuwa zinatoa huduma bora na kuachana na dhana ya kwenda kutibwa nje ya   nchi.

Akizungu na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali hiyo  Daktari bingwa wa magonjwa ya saratan ,Dr  Harrison  Chuwa amesema kumekuwa na tabia na mazoea  kwa baadhi ya watu kuamini kuwa huduma bora za afya zinatolewa  ughaibuni nawamejikuta wakitumia gharama kubwa nausumbufu wa safari .

,,Hospitali yetu inatoa huduma bora sana ukilinganisha na hizo wanazokimbilia huko India kwenda kutibiwa, nataka niwaambie kwamba Hospitali ya Agakhan ina wataalamu na vifaa vya kutosha  ndiyo maana tumepata tuzo  ya kima taifa ya  GSI tuzo hii kuna hosptali ziko huko india na hazijawahi kipata hata maramoja ,sisi ni wa kwanza nchini , wapili Afrika ya Mashariki na watisa Afrika kwa ubora wa utoji huduma ,, alisema Dr Chuwa.

Aidha dr Chuwa amwataka wananchi kujenga utamaduni wa kupima afya na kuacha kusikiliza maneno ya pembeni kuwa hospitali hiyo kwamba ina toza gharama kubwa ,na kufuta dhana kwamba hospitali hiyo wanatibiwa tu watu wenye uwezo(vigogo).

Kwaupande wa huduma za magojwa ya moyo ,dr Lucy Odhiambo ni meneja wa wa kitengo cha wagonjwa wa dharura  (ICU) amesema  Agakhani ina toa huduma kwa wagonjwa wa moyo na hudumahizi mgonjwa  akishafika ndani ya dakika 20 mgonjwa anakuwa amesha onana na Dactari, na huduma hii inatolewa kitaalam na kutoka na  ugonjwa  huu kusmbua watu wengi  maranyingi kwamwezi wamekuwa wakihudumia wagonjwa wa moyo zaidi ya hamsini na  wagonjwa zaidi ya 300 wametibiwa kwa muda wa miezi mitatu wakiwemo wagonjwa kutoka nje ya nchi.

,,tulipata mgonjwa wa dharura  alitumwa na nchi yake kuja kusoma hapa nchini  lakini akaugua wakamleta hapa kwetu tulinhudumia  mirija ilikuwa imeziba tuka mtibu , na mwingine  mzungu mtalii naye tuka mtibia  na walifurahia huduma zetu”

Bima ya afya
Khalifa Rehani kutoka Jubilee Insurance ,mesema wameiamini Hospitali  Agakhani  kwa kuruhusu wateja wake kutibiwa hapo  kwa kuwa wameridhishwa na hudumazake ,amesema,  kwa kushirikiana na Agakhan mwezi uliopta walizindua huduma ya jilinde afya inayo muwezesha mgonjwa kutibiwa hadigharama ya shilingi million hamsini ,kitu ambacho bahdi ya bima hazifnyi hivyo, jublee italipavipimo ,matibabu ,kumuna daktari, na naruhusu mteja kupma afy yake hatakama haumwi ,na inatoa maternity ,kujifungua kwa kawaida au kwa operesheni, na haina muda wakusubiri ukukata bima hiyo siku hiyohiyo uanaanza kuhudumiwa .

,,Tumeamini Agakhani kwasababu wanatoa huduma za kuaminika  hawaja wahi kukosa dawa wao wana oda zadawa kutoka kiwandani hivyo kuishiwaq dawa kwao si rahisi wateja wetu wana kuwa salama zaidi muda wote”


Naye afisa masoko na mawasiliano wa Hospitali hiyo bwana Olayce Lotha amesema ,Hospitali hiyo ina pokea wagonjwa wandani na kutoka nje ya nchi , kama Congo,Comoro, Kenya, na kutoka visiwani Zanzibar,na katika kitengo chao cha  Saratani wana pokea wagonjwa  wa saratani na wamekuwa wakifanyiwa matibabu  bora  ikwemo matibabu ya kemikali (chemotherapy) katika kuhakikisha jamii inapata uelewa juu ya saratani Hospitali ya Agakhani kwa kushirikiana na Taasisi ya saratani Oceanroad  na Hotel ya Baharibeach  wameandaa matembezi ya hisani ya takayo fanyika  tarehe  29 oktoba  mwaka huu.

,,pia tunafanya upanuzi wa Hospitali ilikuongeza  na kupanua huduma zetu  sasatuna uwezo wa kulaza wagojwa 74 na majengo mapya yakikamilika tuta kuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 170”


No comments