UHABA WA WATUMISHI MABARAZA YA ARDHI YA WILAYA KUNASABABISHA MSONGA MANO WA MASHAURI
Kaimu Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, Bibi. Amina Rashid Ntibampemba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Mabaraza hayo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mboza Lwandiko.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Mboza Lwandiko akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hali ya Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya leo Jijini Dar es Salaam
Na Maria kaira
Na Maria kaira
mwabawahabari
Kutokana na Changamoto zinazozikabili mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya yamechangia kuchelewesha ukaguzi katika maeneo ya migogoro kutokana na ukosefu wa usafiri hali inayopelekea kasi ndogo ya utendaji kazi.
Serikali imetakiwa kuhakikisha inaboresha mabaraza hayo kwa kuongeza kasi ya kuunda mabaraza mapya ili kupunguza adha zinazozipata wananchi pindi wanapotaka huduma kutoka katika mabaraza hayo.
Kwa kufanya hivyo mabaraza yataweza kuwaondolea wananchi kero za migogoro ya ardhi na nyumba kwa haraka na kwa gharama nafuu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo hii kaimu Mwenyekiti Baraza la Ardhi na Nyumba ya wilaya ya Kinondoni Amina Rashid amesema mabaraza hayo yanakabiliwa na Changamoto ya uelewa mdogo wa wananchi juu ya sheria na kanuni za uendeshaji wa migogoro ya Ardhi.
Amina amesema kutokana na upungufu wa watumishi katika mabaraza hayo umechangia kwa kiasi kikubwa kucheleweshwa kwa kusikilizwa mashauri yaliyofunguliwa na wananchi na kuwalazumu kwenda umbali mrefu kutafuta huduma.
"Kutokana na kasi ndogo ya uundaji wa mabaraza ya ardhi na nyumba ya wilaya inawalazimu wananchi kuangaika kutafuta huduma" amesema
Aidha amesema kuwa mikakati waliyonayo ni pamoja na kuimarisha mabara kwa kuongeza ofisi na watumishi wa kutosha, pia na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu sheria ya mahakama za ardhi ya mwaka 2002 na kanuni za mabaraza.
Post a Comment