Ads

TAHADHALI YA KUTOKEA BAALANJAA NCHI YATOLEWA.




Na:John Luhende 
mwambawahabari
Mamlaka ya hali ya hewa ,idara ya usalama wa  chakula  mifungo na uvuvi na idara ya uratibu wa maafa   kwa  pamoja  wametoa tahadhali kwa wananchi juu ya haliya hewa na chakula nchini kutokana na tishiola ukame unaotarajia kuikumbanchi.

Akizungumza na waandishi wa habari  kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa  Dr Paschal Waniha  amesema muelekeo wa  mvua kwa kipindi cha mwezi October hadi December , kutakuwa na mvua chache  zinazo tarajiwa kunyesha katika maenea machache ya nchi ispokuwa katika  maeneo ya mikoa ya ziwa Victoria pamoja na mikoa ya kusini ndiyo pekee ya natarajiwa kuwa na mvua za kuridhisha.

Aidha ametahadharisha kuwa kuna uwezekano  wa kuwa na mlipuko wa magojwa kutoka na uhaba wa Maji salaama  na mifumo na matumizi ya maji taka katika miji na malisho hafifu ya mifugo na kuwa taka wafugaji wana ishi maenehayo kupunguza mifugo kwa kabla ya athali kubwa kutoka.
Naye mkurugenzi wa idara ya uratibu maafa  ofisi ya waziri mkuu ametoa tahadhali kwa wizara ,taasisi za kiserikali ,mamlaka za mkoa  na wadau wengine wa usimamizi wa maafa  kuchukua hatua muhimu ili kukabiriana na athali hizo,kwa kuhifadhi chakula  vizuri ,kuzuia matumizi ya nataka katika kutengeneza pombe , na kuwahimiza wana nchi kuhifadhi chakula cha kutosha  hasa katika maeneo hali tajwa kuwa kame   .

Pamoja na hayo  idara ya usalama wa chakula   ofisi ya waziri mkuu imemtakawakala wa taifa wa hifadhi ya chakula  kununua na kuhifadhi chakula  cha kutosha  kutoka kwenye maeneo yenye ziada mapema ili kukabiliana na bada la njaa.

No comments