Ads

ADHABU YA KIFO YAPINGWA MAHAKAMANI ,LHRC YASEMA INAKIUKA HAKI ZA BINADAMU




Na John Luhende
Mwambawahabari
Kituo cha sheria na ham za binadamu LHR ,kimetoa  tamko kulaani na kuomba  adhabu ya kifo ifutwe kwa  kuwa imekua ikiathiri kwa kiwango kikubwa haki ya msingi ya kuishi kwa kuwa ni adhabu inayo inayo dhalilisha utu wa binadamu.

Akisoma tamko hilo Leo katika kuadhimisha siku ya kupinga adhabu ya kifo duniani mbele ya waandishi wa habari mkurugenzi mtendaji wa  kituo hicho Bi Hellen Kijo Bisimba , amesema ,wakati umefika Sasa kwa Tanzania  kuachana na adhabu hiyo kwa kuwa hata waingereza walio ianzisha tayari wamesha achana nayo, serikali  itekeleze pendekezo la tathimini ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa kwa kuridhia  mkataba wanyongeza wa haki za kiraia na kisiasa na kutangaza  rasmi Sasa kuwa adhabu hiyo haitekelezeki.



Aidha ameitaka serikali  kurekebisha sheria ya kanuni na adhabu na sheria ya ugaidi yenye kutoa adhabu ya kifo kwa makosa  ya mauaji ,uhaini na ugaidi.


Vilevile  amesema serikali ibadilishe sheria  na kuondoa adhabu ya kifo na kuweka  adhabu mbadala kwenye  akosa ya jinai  na kwa wafungwa  waliopo ,mfano  vifungo vya muda mrefu gerezani .

Pamoja na hayo adhabu hiyo hapa nchi haija tekelezwa kwa muda mrefu ambapo hadi mwaka  2016 kulikuwa na  watu 472 walio kuwa wamehukumiwa kunyongwa  ambao kati yao 452 ni wanaume na  wanawake 20 kati yahao  wanao subiri kunyongwa ni 228 na wengine 244 bwana subiri maamuzi ya  rufani zao , na sheria hiyo haija tekelezwa kwa muda wa miaaka 24 ya kwanza Uhuru  buku watu 72 pekee wameshawahi kunyongwa  yangu sheria hiyokanzishwa.




Pamoja na hayo kituo hicho kimefungua kesi mahakama Mkuu  dhidi ya mwanasheria Mkuu wa Serikali kupiga adhabu hiyo na kuwataka wapigania haki kote nchini kuunga mkono juhudi hizo ili haki iweze kutendeka na kukomesha udhalilishaji huo wa haki ya msingi ya kila binadamu.

No comments