Ads

treni ya jiji haitokuwepo jioni leo februari 09, , 2016


KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL



(TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)


HUDUMA YA TRENI YA JIJI HAITOKUWEPO JIONI LEO FEBRUARI 09, 2016!


Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusitishwa huduma ya treni ya jiji maarufu kama Treni ya Mwakyembe awamu ya jioni ya leo Februari 09, 2016.


Taarifa imefafanua kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na maji ya mvua kuchimba shimo kubwa katika tuta la reli karibu na stesheni ya Buguruni kwa Mnyamani.


Uharibifu huo uligundulika leo asubuhi mara baada ya treni kupita eneo hilo  ikielekea stesheni  ya Dar es Salaam.wakati wa safari yake ya kwanza kutoka Kituo cha Ubungo Maziwa.


Tayari mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio wakiendelea na kazi ya  ukarabati na kwamba inatarajiwa huduma hiyo itarejea tena hapo kesho kama kawaida.


Atakayesoma taarifa hii amuarifu mwenziye.

Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Nd Masanja Kungu Kadogosa
Dar es Salaam,

Februari 09, 2016.





No comments