Serikali yawakutanisha vijana kuunda kanuni za uendeshaji Baraza la Vijana Taifa
Na; Genofeva Matemu
Serikali
imedhamiria kuhakikisha kuwa vijana wanakuwa na chombo chao chenye kujali
utaifa, uzalendo na maslai bila kujali itikadi za kisiasa, kidini, rangi, hali
za kiuchumi, jinsia na maumbile kwa kuandaa kanuni zitakazolifanya Baraza la
Vijana Taifa kuwa huru na lenye haki.
Hayo yamesemwa na
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu Bw.
Eric Shitindi alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa maendeleeo ya vijana
jana jijini Dar es Salaam.
katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa
“Nimuhimu kuunda
Baraza kisheria litakalokuwa na uwakilishi wa vijana wa makundi yote ili liweze
kutumika katika kuleta umoja na mshikamano wa kitaifa” alisema Bw. Shitindi
Aidha Bw. Shitindi
amelipongeza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kutunga sheria
Na. 12 ya mwaka 2015 ya Baraza la Vijana Taifa ambalo litaleta maendeleo ya
vijana na nchi kwa ujumla.
Akizungumza katika
kikao hicho mwenyekiti aliyeteuliwa kuongoza mjadala huo Bw. Godwin Kunambi
amesema kuwa Vijana takribani 120 wamepata fursa adhimu ya kushiriki katika
vijana hao kujadili mambo ya msingi yatakayowawezesha wananchi wa Tanzania
uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa hivyo kuwataka
hususani vijana kutatua kero zao kupitia Baraza hilo.
Naye mwakilishi
kutoka kundi la watu wenye ulemavu Bw. Gaston Hemed Mcheka ameipongeza Serikali
kutoa nafasi kwa kundi la watu wenye ulemavu kuwa na uwakilishi kuanzia ngazi
litatumia nafasi hiyo kutatua changamoto zinazowakabili.
ya kata hadi mkoa pindi Baraza la Vijana Taifa litakapoanza ambapo kundi hilo
Kikao cha wadau wa
maendeleo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza
la Vijana Taifa kimeshirikisha takribani vijana 120 kutoka Mamlaka mbalimbali
kidini, Vijana wenye ulemavu, Shule za Sekondari pamoja na Shule za msingi.
za Serikali, Asasi za kiraia, Vyama vya siasa vilivyosajiliwa, Taasisi za
Post a Comment