Ads

Serikali yapanga kufanya matumizi yenye tija

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango


Na Raymond Mushumbusi 
mwambawahabari

Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 imejipanga kufanya matumizi yeneye tija kwa kuelekeza bajeti kubwa kwenye mambo muhimu hasa sekta zenye za kutoa huduma na zile zenye kuleta maendeleo ya nchi moja kwa moja.
Akiwasilisha mwongozo wa kuandaa mapango na bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Phillip Mpango amesema mwongozo wa  mpango na bajeti umezingatia mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/2017 pamoja na kuzingatia sera za uchumi na hadi sasa sera za bajeti kwa  mwaka 2016/2017 zinaonesha jumla ya shilling trillion 22.9 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika kipindi hiki.
“ Kati ya mapato hayo,serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi ya jumla ya shillingi trillion 14.1 sawa na ongezeko la asilimia 14.1 ikilinganishwa na makadirio ya mwaka 20015/2016, na kwa mapato yasisiyo ya kodi na mapato kutoka vyanzo vya Halmashauri ni shilling trillion 1.1.
“ katika mwaka wa fedha 2016/2017,Serikali tunatarajia kukusanya jumla ya shilling trilllioni 14.1 kutoka kwenye vyanzo vya kodi ,sawa na asilimia 13.2 ya pato la taifa hii ni sawa na ongezeko la asilimia 14 ukilinganisha na matarajio ya kukusanya jumla ya shilling trillion 12.3 kwa mwaka wa fedha 2015/2016” Alisema Mhe. Mpango.
Mhe Philip Mpango amesema mapato yote yatakusanywa na Wizara ya Fedha na Mipango, hivyo basi maafisa,Masuuli,wa Wizara,idara za serikali,Wakala,Taasisi,Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za Mitaa watatakiwa kuwasilisha mapato yote yatakayokusanywa na kuwasilisha kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali na yatagawiwa kulingana na bajeti iliyoidhinishwa.
Aidha amesema Serikali itahakikisha Mashirika ya Umma yaliyoundwa kwa lengo la kujiendesha kibiashara yanajiendesha kwa faida bila ya kutegemea ruzuku ya Serikali, na ameyataja baadhi ya mashirika hayo kuwa ni  Shirika la Umeme(TANESCO),Shirika la Reli ya Tanzania Zambia (TAZARA), Shirika la Reli ya Kati (TRL), Shirika la Ndege (ATCL),Wakala wa Vipimo (WMA), Bodi ya Mazao, na mashirika mengine.
Serikali itahakikisha kuwa inahimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuelekeza matumizi kwenye maeneo yenye tija kwa manufaa ya watanzania wote.

No comments