Na Nyakongo Manyama
mwambawahabarblog
Halmashauri ya Wilaya ya
Butiama Mkoani Mara imesema imepata ufumbuzi wa changamoto ya
wanafunzi wa darasa la kwanza na awali Shule
ya Msingi Mwibagi wilayani waliokosa mahali pa kusomea kwa kuwagawa wanafunzi
hao kwa awamu mbili.
Hayo yamebainishwa leo
(Alhamisi 04, Februari 2016), Afisa Elimu wa Wilaya hiyo, Hans Mgaya, wakati
akizungumza na mwandishi wa habari hii, ambapo alikiri kuwepo kwa changamoto ya
uhaba wa madarasa shuleni kutokana na ongezeko la wanafanuzi walioandikishwa
kuanza darasa la kwanza mwaka huu, ambapo hata hivyo tayari wameshachukua hatua
mbalimbali za kukabiliana na tatizo hilo.
Aidha, Mgaya amesema
kuwa jitihada za muda mfupi walizozifanya ni kuwagawa wanafunzi hao
katika mikondo miwili ili waweze kubadilishana madarasa , mkondo
mmoja utaingia asubuhi na mkondo mwingine mchana.
Kwa mujibu wa Mgaya
alisema jitihada za muda mrefu ni kujenga shule nyingine mpya ili kusaidia
kuchukua wanafunzi wengi kwa wakati mmoja, ujenzi wa shule hiyo ulishaanza
kabla ya tamko la elimu bure na tupo katika hatua ya
awali ya ujenzi wa msingi wa madarasa hayo alisema Mgaya.
“wanafunzi
walioandikishwa kujiunga na shule ya msingi kwa mwaka huu 2016 imeongezeka kwa
kiasi kikubwa hivyo kusababisha idadi ya wanafunzi kuwa kubwa” alisema Mgaya.
Idadi ya wanafunzi wa
darasa la awali na la kwanza walioandikishwa kwa mwaka 2016 katika shule ya
msingi Butiama kuanza masomo, ambapo hata hivyo zaidi ya wanafunzi 240 wa shule
hiyo wanasomea katika chumba kimoja.
Post a Comment