Ads

Mratibu wa Kituo cha Usuluishi cha TAMWA, Bi. Gladness Hemedi Munuo akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati walipokuwa wakilaani vikali ucheleweshwaji na upotoshaji wa kesi za vitendo vya ukatili. 
Na John Luhende
Kutokana na  kuongezeka kwa matukio ya unyanyasaji na ubakaji  nchiniChama cha waandishi wa habari wanawake  TAMWA   kimetoa tamko kuhusiana na mwenendo wa waripoti  za matukio hayo yaliyo ripotiwa Polisi na kufungulwa kesi  mahakamani na kusema kuwa  chamahicho hakilidhishwi na jinsi matatizo hayo yanavvyo shughulikiwa.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es saaam mkurugenzi mtendaji wa TAMWA  bi Edda Sanga  hatua hiyo  imekuja mara baada  ya TAMWA  kubaini kuwa kesi 62  za ubakaji kushindwa kutolewa  hukumu na maamuzi katika mahakama mbalimbali jijini Dar es salaam katika kipindi cha mwaka 2014 -2015  kati ya kesi 63 nikesi mojatu  mtuhumiwa amehukumwa kifungo cha miaka  30 jela,kesi 43 ziko mahakamani,kesi 7 zimeshindwa kufika mahakamani ambapo kesi mbili zimefutwa kwa kukosekana ushahidi.

Amezitaja taja  Mahakama zinazolalamikiwa kuwa ni pamoja na  Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ,Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Ilala na temeke   na kwa upande wa Hospitali baadhi ya madaktari wamekuwa  wamekuwa wakiwa omba Rushwa walala mikaji na waathirika  iliform zao za pf3 zijazwe sahihi,sanjari na hilo badhi yao wame lalamikiwa kwa kupokea pesa  kutoka kwa watuhumiwa ili wapotoshe ukweli,Chama hicho kinaunga mkono  tamko la mh Ra John  Magufuli  alilo litoa siku ya sheria Duniani linalo sema kila hakimu  wa mahakama anapaswa  kuhukumu kesi 260 kwa mwaka na ahukumu  kwa haki.
Mtoto akitoa ushaidi ni kwa jinsi gani alivyofanyiwa kitendo cha ukatili wa kijinsia.
Mwanasheria wa TAWLA, Mary Richard (wa kwanza kulia) akizungumza ni kwa jinsi gani wanavyowasaidia wanawake wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia leo katika mkutano na waandishi wa habari leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga(katikati) akizungumzia mbele ya waandish wa habari (hawapo pichani) ni kwa jinsi gani wamepata malalamiko kutoka kwa familia zinazofanyiwa unyanyasaji wa kijinsia hasa ubakaji na ulawiti katika ngazi za mahakama, polisi na baadhi ya hospitali hapa nchini.

No comments