MSANII WA FILAMU ROSE NDAUKA NA MENEJA WAKE WAZINDUA JARIDA LITAKALOKUWA LIKITOKA KWA WIKI MARA MOJA
Msanii wa Filamu nchini, Rose Ndauka (kushoto) na Meneja wake Ramaehan Mwanana wakionesha Jarida jipya litakalojulikana kama Rozzie Magazine wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Meneja wa Ndauka Ramaehan Mwanana (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Rose Ndauka, akizungumza katika uzinduzi huo.
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
MSANII wa filamu Tanzania, Rose Ndauka amezindua jarida jipya liitwayo Rozzie litakalotoka mara moja kwa kila mwezi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, wakati wa uzinduzi huo, Rose alisema dhumuni kubwa la jarida hilo ni kuelimisha, kuiburudisha, kuikosoa na kuichochea jamii katika kufikia malengo yao ya kimaisha kwa ujumla na kujenga taifa bora lenye maendeleo.
“Pia katika kurasa za ndani za jarida hilo zipo kurasa zilizobeba mambo ya fasheni, maisha pamoja na mambo mbalimbali yanayoikosoa jamii pale inapokosea,” alisema.
Alisema kuwa lengo la kutoa jarida hilo ni kuwafikia watanzania wote na nakala yake itapatikana kwenye mtandao ya kijamii mara moja kwa kila wiki.
Alisema magazine hiyo anaitoa bure kiwa watanzania wote na litakuwa likitoa taarifa taarifa mbalimbali kwenye mitandao yote ya kijamii ambayo ni Facebook, Instagram, Twitter na You Tube.
Meneja wa jarida la Rozzie, Ramadhani Mwanana, alisema wameanza kwa kuchapisha kopi 5,000 na jinsi wanavyoendelea waziongeza nyingi zaidi.
Alisema jarida hilo ltasambazwa katika mikoa yote hapa nchini kwa kutumia magari makubwa ya mikoani, maduka mbalimbali pamoja na nyingine zitakazowezesha watanzania kupata magazine hiyo.
Post a Comment