Ads

MKE WA RAIS MAMA MAGUFULI AMEWAOMBA WADAU MBALIMBALI KUSAIDIA WAZEE NA WATU WASIOJIWEZA


Na Magreth Kinabo
 mwambawahabariblog
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Janeth Magufuli ameziomba na kuzimahamasisha taasisi za Serikali na zisizo za Serikali kushirikiana na Serikali kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu Wasiojiweza kijulikanacho kwa jina la Nunge,viwemo vingine.

Aidha alisema vituo hivyo  jumla vipo 17, katika maeneo  mbalimbali nchini.
 Kauli hiyo imetolewa leo na Mama Magufuli wakati alipotembelea makazi hayo yaliyoko Kigamboni eneo la Vijibweni jijini Dares Salaam, ambapo  alisema changamoto wanazokabiliana nazo  amezisikia na na aliwaahidi kuwa  atashirikiana na wadau wote kuzitafutia majibu yake.

Mama Magufuli alizitaja baadhi ya  changamoto hizo, ni kuwa uchakavu wa miundombinu, uhaba wa rasilimali fedha na watu, pamoja na maslahi duni ya watoa huduma, upungufu wa vitendea kazi na huduma za jamii, pamoja na uvamizi wa eneo la kituo.
Aidha Mama Magufuli alimwomba Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema kulishughulikia taizo la uvamizi wa eneo hilo na kulitafutia ufumbuzi.

“ Natumainni  zawadi  tuliyoileta ni ndogo na haiwezi kumaliza matatizo yote mliyonayo. Lakini ni matumaini  yangu kuwa zawadi hii inaweza kuwa chachu ya kuhamsha hamasa ya watu na vikundi vingine kujitoa kusaidia watu wasiojiweza.  Ni imani  yangu kuwa endapo watu wote tutajitoa  kwa dhati tutaweza kuwahudumia wazee na watu wasiojiweza na hivyo kuwapunguzia  makali ya maisha . Tukumbuke ‘kutoa ni moyo na si utajiri’ na kwamba “sisi sote ni wazee na walemavu watarajiwa”.

Aliongeza kwamba ni  dhahiri kuwa Serikali ina wajibu mkubwa katika kuhudumia wazee na watu wasiojiweza. Hata hivyo Serikali pekee haiwezi kumaliza matatizo yote yanayowakabili na wazee na watu wasiojiweza.
 Hivyo basi, sote kwa pamoja tunao wajibu wa kusaidia nguvu za  Serikali  katika kuwahudumia watu hao.

“Na kwa kutambua hilo , mimi  na wenzangu  niliombatana nao  tumeamua kutoa zawadi yetu ndogo kwenu. Zawadi  hiyo inajumuisha vitu vifuatavyo mchele kilo 3000, unga kilo 3000 na maharage kilo 1200. Kulingana na idadi yenu niliyopewa kila mmoja atapewa kilo 25za mchele, kilo 25 za unga na kilo 10 za maharage.

“Nawaombeni mniruhusu pia kuchukua nafasi hii kuwasilisha kwenu salamu nyingi kutoka kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ameniomba niwaarifu kuwa yupo pamoja nayi na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wazee na watu wasiojiweza wanapata huduma zote muhimu kwa kadri ya uwezo wake,” alisisitiza  Mama Magufuli.

Mama Magufuli aliongeza kwamba wazee na watu wasiojiweza wanahitaji upendo, kuthaminiwa nakusaidiwa.Hivyo kipimo kimojawapo cha kupima jamii iliyostaarabika na inayoheshimu misingi ya utu ni kuangalia namna inavyo wathamini wazee na watu wasiojiweza.

Aliupongeza uongozi na watumishi wote wa kituo hicho na vituo vingine nchini kwa kazi kubwa wanayoifanya licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa.
 Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke , Sophia Mjema alimtaka kila mwananchi kutambua kwamba bila wazee hakuna tutakachoweza kufanya hivyo ni muhimu kuwa enzi na kuwasaidia wazee walioko majumbani na mitaani.

“ Tuwaenzi wazee na kuwasaidia pia hata wale walioko mitaani tuwashauri warudi majumbani ili Serikali iweze kuwaorozesha kwa kuwa si vizuri kukaa barabarani, Serikali ya Awamu  ya Tano ya Rais Magufuli itahakikisha inawajali wazee,” alisema.
 Akizungumzia kuhusu watoto wa mitaani alisemani wajibu wa wazazi kuhakikisha wanawalea watoto wao vizuri ili wasikilimbile mitaani kwa kuwa watoto ni taifa la kesho.
Naye Mwenyekiti wa wazee wa makazi hayo, Anthony Kikongoti alimshukuru Mama  Magufuli kwa niaba ya wenzake, kwa kuanza ziara yake ya kwanza ya kutembelea kituo hicho ,ambapo alimwomba apeleke salamu zao kwa baba  yao ambaye ni Rais Magufuli kuwa wanasema asante.
“Huu ni mwaka wa wanyonge dini zote tumwombee kwa pamoja ili aweze kuendelea kupunguza makali ya maisha,” alisema.
 Afisa Mfawidhi wa kituo hicho, Ojuku Mgedzi alisema wanahitaji bajeti ya kutosha ya kuendesha shughuli mbalimbali, watumishi 42 , wakiwemo walinzi, kwa kuwa waliopo sasa ni 29 na  hawatoshi.

Alisema eneo hilo lina hekari 50.8 na nusu ya eneo hilo limevamiwa.
Mgedzi alisema kituo hicho kina idadi yawakazi 112, ambapo alimkabidhi Mama  Magufuli orodha ya idadi ya watu hao.
Mwisho.

No comments