Mauzo ya soko katika soko la hisa
Idadi ya mauzo imeongezeka zaidi ya mara 3 hadi Bilioni 11.3 kutoka Bilioni 3.5.
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa pia imepanda zaidi ya mara 18 hadi Milioni 13.1 kutoka Laki 7.
Kampuni tatu zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni zifwatazo:
1. CRDB kwa asilimia 96.43%
2. TBL kwa asilimia 3.09%
3. NMB kwa asilimia 0.16%
Idadi ya Mtaji wa Soko
Ukubwa wa mtaji wa soko umepanda kutoka Trilioni 20.1 hadi Trilioni 20.8 wiki hii.
Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umebakia kwenye kiwango kile kile cha Trilioni 9.
Viashiria (Indeces)
· Kiashiria cha sekta ya viwanda kimepungua pointi 32.56 kikiwa kimechangiwa na punguzo la bei ya hisa kwenye kaunta za TCCL (7.66%), TCC (2.48%) na TOL (0.65%)
· Kiashiria cha sekta ya huduma za kibenki na za kifedha kimeshuka pointi 92.94 kikiwa kimechangiwa na punguzo la bei ya hisa kwenye kaunta za NMB (7.33%) na DCB (0.89%).
· Kiashiria cha sekta ya huduma za kibiashara kimeshuka pointi 75.34 kikiwa kimechangiwa na punguzo la bei ya hisa kwenye kaunta ya SWISSPORT (2.61%)
Post a Comment