Serikali kuanzisha Vyuo vya Uvuvi kuongeza ujuzi kwa vijana
Na Raymond Mushumbusi- Dododoma
mwambawahabari
Serikali imekusudia
kuanzisha Vyuo vya Uvuvi katika maeneo yote yanayozungukwa na bahari ili
kuwafundisha vijana mbinu sahihi za kufanya shughuli za Kilimo,Mifugo na Uvuvi
ili kuwawezesha kukuza vipato vyao kwa kujiajiri.
Hayo yamesemwa leo
Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Mhe.William Tate Ole Nasha akijibu swali la Mhe. Hamidu Hassan
Bolali Mbunge wa Mchinga (CUF) kuhusu umuhimu wa kujenga chuo cha uvuvi mkoani
Lindi ili kuwaongezea vijana ujuzi wa kazi hiyo.
Ameongeza kuwa wizara
inatambua umuhimu wa kuwafundisha vijana mbinu sahihi za kufanya shughuli za
uvuvi kilimo na ufugaji na kwa sasa wizara kupitia Wakala wa Elimu
na Mafunzo ya Uvivu (Fisheries Education and Training Agency (FETA) imeanzisha
Chuo cha Uvuvi Mikindani Mtwara kwa lengo la kusogeza huduma ya mafunzo ya
uvuvi kwa wananchi hususani vijana walioko ukanda wa kusini mwa Tanzania
ukiwamo mkoa wa Lindi.

Mhe.William Tate Ole
Nasha amesema uanzishwaji wa Vyuo vya Uvuvi sio kwa maeneo yanayozungukwa na
bahari ila kwa maeneo mengine pia ili kuwezesha vijana kupata ujuzi zaidi sio
katika uvuvi pekee bali pia katika kilimo na ufugaji, mbali na Chuo cha Uvuvi
Mikindani Mtwara pia kuna vyuo vingine kama vile Chuo cha Mbegani
Mtwara chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 120 , Chuo cha Kibilizi
Kigoma na Chuo cha Nyegezi Mwanza.
Mbali za Vyuo hivyo
serikali imehaidi kujenga vyuo Tanzania nzima ili kuwawezesha vijana wengi
zaidi kupata kupata ujuzi zaidi katika Kilimo, Uvuvi na Ufugaji ili kuendeleza
ukuaji wa sekta hiyo na kuwezesha vijana kujiajiri wenyewe kupitia mafunzo
wanayapata.
Wakala wa Elimu na
Mafunzo ya Uvuvi (FETA) itaanza kutoa mafunzo ya uvuvi katika Chuo cha Uvuvi
Mikindani ya muda mfupi kwa mwaka 2016/2017 na yale ya Astashahada na
Stashahada yataanza mwaka 20017/2018.
Post a Comment