Na John Luhende
mwambawahabariblog
Waandishi wa habari
nchini wametakiwa kuandika habari za
kuelimisha jamii kuhusu masualambalimbali ya kuelimisha jamii ikiwemo sector ya mafuta na gas badala ya
kuandika habari za uchochezi wa migogoro katika jamii
Hayo yalisemwa na mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam mh sadiq meck
sadiq alipo kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa semina semina iliyo andaliwa na shirika la petrol Tanzania
TPDC kwaajli ya kuwajengea uwezo
waandishi wa habari kuandika za ukweli kuhusu sector ya mafuta na gas nchini .
Naye mkurugenzi mkuu wa shirika hilo bw James
Mataragio amesema nijukumu la waandishi
wa habari na wataalamu kuwaelimisha wananchi
kuhusu habari za maendeleo ya mafuta nagas nchini , na ameongeza kuwa watanzania wanatakiwa kuelewa kuwa miradi ya mafuta na gas ni miradi
mikubwa na mtokeo yake yana onekana kwa
muda murefu na wawe wavumilivu .
Pamoja na hayo alisema kuwa kwasasa ni takribani viwanda 37 nchini vinatumia nishati ya gas asilia na taasisi mbalimbali na hivi karibuni mradi wa usambazaji wa gas ya majumbani kwa kutumia mabomba utaanza na
nyumba 36000 zita patiwa huduma hiyo
kwa awamu ya kwanza
Post a Comment