Ads

KISARAWE CEMENT YATOA MSAADA WA MIFUKO 200 YA SARUJI WILAYANI KINONDONI

 Na:John Luhende 
mwambawahabariblogspot
Mkuu wa wila ya Kinondoni  mh Paul Makonda  leo amepokea  msaada wa mifuko 200 ya saruji kutoka kampuni ya Kisarawe   cement inayotengeneza cement ya  Lucky ,itakayo saidia kujenga shule katika wilaya hiyo ambapo  kwa mujibu wa mkuu huyo  wanakusudia kujenga  shule saba  ili kuka biliana na tatizo la watoto kukosa shule 
 linalo ikabili Wilaya  hiyo.




Akizungumza  katika tukio hilo mh Makonda amesema wilaya hiyo ina upugufu wa shule saba za kata ambapo mwaka jana wanafunzi wapatao 3183, walikosa nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza, ameongeza kuwa Kinondoni imefanya vizuri katika mtihani wa taifa wa kidato cha pili ambapo  katika shule kumi bora imetoa shulenne.


Naye mkurugenzi wa  mapato na mauzo wa kampuni bi;Florence Mshakangoto mara baada ya kukabidhi msaada huo amesema wao  kama kampuni wameguswa na tatizo hilo na ameahidi kuendelea  kuchangia huduma muhimu  za jamii zikiwemo shule ili kuinua kiwango cha elimu ya watoto wa Tanzania ,na kuwaomba wafanyabiashara wengine kuchangia   wilaya hiyo





No comments