BAWATA waunga mkono tamko la Serikali
Mkurugenzi wa Baraza la Waganga Tanzania (BAWATA)David Wiketye akiongea na waandishi wa habari kuhusu waganga wanaokiuka taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali juu ya utoaji huduma ya tiba asili nchini, kulia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Shaka Mohamed Shaka.
Picha na Beatrice Lyimo
Jacquiline
Mrisho
mwambawahabariblog
Baraza la Waganga
Tanzania (BAWATA) wameunga mkono tamko la Serikali la kukataza waganga wa tiba
asili kujitangaza katika vyombo vya habari.
Hayo yamesemwa leo
jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Waganga Tanzania Shaka Mohamed
Shaka alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu waganga wanaokiuka
taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali juu ya utoaji huduma ya tiba asili
nchini.
‘’Sisi kama Baraza la
Waganga Tanzania tukishirikiana na Serikali tunatoa wito kwa vyombo vya habari
wasitoe matangazo ya waganga wa tiba asili kwakua jambo hili ni kosa kwa mujibu
wa sheria”alisema Shaka
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Baraza hilo David Witekye ameiomba radhi Serikali kutokana na
tamko la Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili Tanzania
(SHIVYATIATA) Abdulraham Lutenga kwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari
bila kushirikiana na kamati yake tendaji wala vyama vinavyounda shirikisho hilo
na kuwatetea wafanyabiashara wa tiba asili ambao wamejivika kilemba cha utabibu
asili.
“kwa niaba ya BAWATA,
tunaiomba radhi Serikali kutokana na tamko la Mwenyekiti wa SHIVYATIATA kupinga
tamko la Serikali, tunaamini lile ni tamko lake binafsi na sio la shirikisho”.
alisema Wiketye.
Ameongeza kuwa,wameafiki
tamko la Serikali kuhusu upimaji na usajili wa dawa asili na kupendekeza zoezi
hili kuangaliwa upya ili kuwezesha watabibu asilia kumudu gharama hizo.
Tamko hilo lilitolewa
baada ya kujitokeza kwa changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoa huduma
wa tiba za asili kutozingatia Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali
inayohusu afya ya jamii.
Post a Comment