Ads

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA 82 DUNIANI KATIKA UHURU WA KIUCHUMI

mkurugenzi mtendaji wa shirika la Uhuru Initietivefor polcy and Education(UIPE) Isaac chungu Danford akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam (picha na John luhende)

Na John Luhende 
mwambawahabariblog
Kwamaranyingine Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi  100 ambazo ziko huru kiuchumi   ikiwa imeshika nafasi ya 82 huku rushwa na udhibiti
wa biashara  vitajwa kuwa kikwazo kwa uchumi  wachi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la  Uhuru Initietive for policy and Educaton(UIPE) bw Isaac Chungu Chungu Daniford amesema tarifa hizo ni kwamujibu wa wariport ya uhuru kiuchumi  iliyo tolewa na umoja wa mashirika yasiyo ya kiserikali  ujulikanao kama uhuru wa kiuchumi  chini ya taasisi  ya Fraster kutoka nchini Canada.

Aidha amesema Tanzania  imepanda nafasi  kumi katika Riport yamwaka huu kutoka nafasi  ya 92  katika riport ya  mwaka 2014 huku Kenya iliyokuwa ikiongoza kwa Afrika mashariki ikiendelea kushuka hadi nafasi ya 66 dunian  na Rwanda  inaongoza katika nchi za jumuiya ya Afrika mashariki kwakushika nafasi ya 34 duniani ikifuatiwa na Uganda inayo shika nafasi ya 40 .

Amezitaja sabababu kuu zinazo zinazo changia kubomoa uhuru wa  kiuchumi nchini kuwa ni  rushwa ,urasimu , mahitaji ya kiutawala, ulazimishwaji wa kuchangia huduma za kiserikali,makubaliano ya mishahara mfumo wa kisheria na  na umiliki wa mali binasi , uaminifu kwa polisi ,usimamizi wa mikataba ya  kisheria.

 Riport hiyo imejikita Zaidi kwenye  takwimu zilizo kusanywamwaka 2013 (mwaka wa karibu Zaidi katika upatikanaji wa taarifa husika) nchi na mamlaka zilizo ongoza  katika kumi bora ni pamoja na Honkong, inayoendelea kushika usukani,Singapore New Zealand,Switzerland,united Arab Emirates  Mauritius Jordan,Ireland nd Canada  huku Uingereza na Chile wakishiha nafasi ya kumi kwa pamoja

 Na nchi zilizo shika nafasi kumi  za mwisho Dunia  ni Angola ,Jamhuri ya afrika ya kati,Zimbabwe, Argentina,Syrya, Chad Libya,Jamhuri ya Congo na  na Venezuela na baadhi ya nchi ambazo hazikupimwa kutokana na ukosefu wa taarifa   ni pamoja na Korea ya kusini na Cuba.




No comments