Ads

KAMANDA KOVA KUSTAAFU LEO KULITUMIKIA JESHI LA POLISI TANZANIA

mwambawahabariblog
 
Na John Luhende
Kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova,leo anastaafu rasmi kulitumika jeshi la Polisi Tanzania  kwa kuwa muda wake kwa mujibu wa
sheria wa kufanya  kazi umeisha.

 Kova ametoa taarifa hiyo leo asubuhi alipokuwa akizungumzakatika kipindi cha kumekucha cha ITV, na kusema kuwa mkataba wake na jeshi la Polisi umeishia leo, hivyo analazimika kukaa pembeni.

"Mmepata bahati sana, maana wakati nakuja Dar es salaam mwaka 2008 nikitokea Mbeya, kwa mara ya kwanza nilifanya kipindi hapa na leo hii nawaagia hapa, leo ndio siku ya mwisho kwangu kulitumikia jeshi la Polisi, mkataba wangu na jeshi la Polisi unaisha leo, lakini siwaachi hivi hivi, Kaimu wangu yupo atakuwa nanyi", alisema Kamanda Kova.

No comments