Ads

TAASISI YA MIFUPA MUHIMBILI MOI YAKANUSHA MGONJWA WA MAGUFULI KUTELEKEZWA


Kaimu mkurugenzi  wa tiba taasisi ya mifupa MOI  DR Samwel  (katikati) Swai akizungumza na waandishi wa habari (picha na John  Luhende)
 Kutokana na habari iliyotolewa na gazeti la Uwazi la tarehe 29/12/2015 ukurusa wa 3 yenye kichwa cha habari ‘Aliyetoa siri Muhimbili kwa Magufuli alazwa chini’’. Uongozi wa Taasisi unauarifu umma kwamba habari hiyo ni upotoshaji kwani mwandishi hakufanya mahojiano na Taasisi ya MOI lengo ikiwa ni kuchafua jina zuri la Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI)
Mgonjwa Chacha Makenge (39) mwenye jalada namba B00269868 ambaye alikua akiishi kwenye handaki maeneo ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam alipokelewa MOI tarehe 18/09/2015 baada ya kudai kushambuliwa na kujeruhiwa kwenye uti wa mgongo ambapo alipata matibabu ya Msingi na aliruhusiwa tarehe 20/11/2015 baada kuonekana afya yake imetengamaa
Baada ya Kuruhusiwa, Bwana Chacha alikataa kuondoka wodini huku akitoa sababu mbalimbali ambazo kimsingi hazikuwa za msingi kimatibabu. Aidha Taasisi kwa kushirikiana na vyombo vya dola ilibaini kwamba bwana Chacha hakuwa na makazi maalum na alikua ametelekezwa na ndugu zake wodini hivyo kuitegemea hospitali kwa huduma zote ikiwemo gharama za matibabu,malazi na chakula
Pamoja na mambo mengine, Taasisi iliamua kumsaidia kwa kutoa fedha kwaajili ya kumsafirisha kwenda Kwao Mkoani Mara wilaya ya Serengeti kijiji cha Mugumu ambapo bwana Chacha alipewa taarifa na kuafiki na taratibu za safari zilifanyika .Katika hali isiyo ya kawaida bwana chacha alikataa kusafiri na kuondoka wodini na hivyo kuitia hasara Serikali ya Shilingi 33,000 ambazo zilitumika kukata tiketi
Mnamo Tarehe 17/12/2015 ndugu Chacha Makenge alipokelewa kwa mara nyingine katika idara ya wagonjwa wa dharura (Emergence) akiwa na rufaa kutoka kituo cha afya cha Magomeni akidai kuwa na maumivu makali ya kichwa na Mgongo ambapo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina na vipimo  madakatari walibaini hakuwa na tatizo lolote
Aidha, Madaktari walishauri apumzishwe wodini(wodi 18) kwa uchunguzi zaidi .Baada ya kufika wodini ndugu Chacha alianza kukiuka taratibu za hospitali kwa kutotimiza wajibu na kuamua kulala kwenye sakafu wakati kwa sasa MOI hakuna Mgonjnwa anayelala chini kutokana na vitanda 300 vilivyotolewa na Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli

Mwisho, Taasisi ya MOI inakemea mwenendo wa mgonjwa huyu wa kukiuka taratibu kwa kulala kwenye sakafu, Kuifanya wodi makazi yake na kuingiza mwandishi wa habari wa gazeti la Uwazi na  kupiga picha wodini   bila idhini ya hospitali kwa lengo la kupotosha umma na kuchafua jina na taswira nzuri ya MOI.
 Mgonjwa  Chacha Makenge akiwa amlala katika kitanda katika wodi ya Sewa Haji MOI  Muhimbili



Vitanda katika wodi ya sewa Haji vikiwa havina wagonjwa kutokana na wingi wa vitanda baada ya mh Rais wa Jamhuri ya Muungano John Magufuli kununua vitanda 300 katika hospital hiyo ( picha zote na John Luhende )



Muuguzi mkuu wa wodi no 18 Rider Rose Rutaguza akiwa andika jina la ke waandishi wa habari marabaada ya kuzungumza nao

No comments