Ads

Kesi ya wafanyakazi wa TRA kusikilizwa Januari 13 Mwakani

Na Nyakongo Manyama                                                                                            
mwambawahabariblog                                                                                                       
Kesi inayowakabili wafanyakazi wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) inatarajiwa kusikilizwa tena January 13, 2016

Akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini dar es salaam Wakili wa Serikali Bi.Dianna  Lukondo amesema kuwa  kwa leo Kesi ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na kutoa dhamana kwa washtakiwa na hivyo imeshindikana kusikilizwa kutokana na upelelezi kutokamilika.

“Upelelezi haujakamilika hivyo kesi itasikilizwa tena Januari mwakani ” alisema Dianna.

Kesi hiyo inawakabili aliyekuwa  Naibu Kamishna TRA  Tiagi Masamaki, meneja wa kitengo Huduma kwa Wateja  Habibu Mponezya, na wengine ni  Khamis Omary, Eliaichi Mrema, Burton Kaisi, Harun Mpande na Raymond Louis.

Washtakiwa hao wanatuhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi, wakidaiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329 katika Bandari ya Dar es Salaam yaliosababisha  ukwepaji wa ushuru zaidi ya sh. Bilioni 80.

No comments